Msemaji wa Chelsea ameweka bayana wameshawasilisha malalamiko yao ili hatua zichukuliwe dhidi ya Clattenburg ambaye amekumbana na ukosoaji mkubwa kwa kile kinachoelezwa ni kushindwa kuumudu mchezo huo.
Chama cha Waamuzi wa Kulipwa PGMO kimekiri kupokea malalamiko hayo na
kusema watayafanyia kazi kwa kadri ambavyo itaonekana na uchunguzi
utafanyika ili kubaini iwapo Clatternburg alitoa maneno ya kibaguzi kwa
Mikel Obi. Katika mchezo huo Manchester United ilivunja mwiko wa kushindwa
kupata ushindi kwenye michezo ya Ligi Kuu katika uwanja wa Stamford
Bridge kwa kipindi cha miaka kumi baada ya kuibuka na ushindi wa magoli
3-2.
Chelsea ililazimika kumaliza ikiwa na wachezaji tisa baada ya
kushuhudia Branislav Ivanovic na Fernando Torres wakilimwa kadi nyekundu
kitu ambacho kilizusha lawama za kila mara kwa mwamuzi Clattenburg.
Manchester United ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa
David Luiz ambaye wakati anaokoa akaukwamisha mpira wavuni kabla ya
Robin Van Persie kufunga goli la pili na kushuhudia Juan Mata akifunga
goli la Chelsea kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Chelsea waliongeza kasi na kufanikiwa kupata goli la
kusawazisha kupitia Ramires kabla ya Javier Hernandez hajafunga goli la
tatu na la ushindi dakika kumi na tano kabla ya mchezo kumalizika na
kuiba ushindi Manchester. Goli la Hernandez lilizidisha hasira kwa wachezaji wa Chelsea na hata
mashambiki wake kutokana na kudai mfungaji alikuwa kwenye eneo la
kuotea na halikustahili kuwa goli na kushuhudia Mikel Obi akilimwa kadi
ya njano kwenye malumbano hayo.
Kwa matokeo hayo sasa Chelsea inaendelea kuongoza kwa tofauti ya
pointi moja baina yake na Manchester United ambayo imepiteza michezo
mieili tangu kuanza kwa Ligi msimu huu na huu ukiwa mchezo wa kwanza kwa
The Blues kufungwa.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII