Joshua Nassari akanusha kufyatua risasi jana kwenye uchaguzi wa madiwani Daraja II Arusha


Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mh Joshua Nassari amekanusha tarifa zilizoandikwa na magazeti ya Uhuru na Habari Leo kuwa jana alifyatua risasi na kuzua tafrani katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha uliofanyika jana.

Nassari ameyasema hayo leo jioni wakati akihutubia kuzindua Kampeni nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa kwa ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.

Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na watu wengi, umefanyika katika viwanja vya Ngaresero Usa-River. Mbali na Nassari, kiongozi mwingine wa Chama aliyehudhuria alikuwa Henry Kileo, kutoka CHADEMA Kanda ya Kinondoni.

Nassari amedai kuwa yeye alikuwa Wakala Mkuu Kata ya Bangata, na kwamba ameshazungumza na OCD kuhusiana na taarifa hizo. Amedai kuwa mtu aliyefyatua risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na kwamba Polisi walimuweka ndani na kuandika maelezo yake...lakini anashangaa kuambiwa ni yeye!!
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs