Joshua Nassari, ametoa siku 14 kwa magazeti mawili kumsafisha

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ametoa siku 14 kwa
magazeti mawili yatolewalo kila siku nchini kumsafisha kwa uzito
waliotolea habari ya kumhusisha kufyatua risasi kwenye kata ya Daraja
Mbili wakati wa uchaguzi mdogo, vinginevyo atayashitaki Baraza la
Habari Tanzania (MCT).
Akizungumza na vyombo vya habari jijini hapa jana, alisema ameshangazwa
kuona propaganda chafu dhidi yake zikiendeshwa kwa wazi na chuki kubwa.
“Mimi nilipita eneo la kupigia kura saa mbili kamili asubuhi nikaend
kata ya ya Bang’ata wilayani Arumeru nikiwa kama wakala mkuu, kusimamia
uchaguzi na tukio hili la kufyatua risasi limetokea mchana saa saba,
nashangaa naandikwa mimi,” alisema.
Alisema kuwa kikubwa anachokiona ni kumpaka matope kupitia magazeti hayo.
Nassari alisema kuwa anachofahami fika magazeti hayo kupitia waandishi
hao wanatumiw ana watu kumchafua kwa sababu wanazojua wao, kufuatia
kushinda uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
“Kwa kweli sasa sitakubaliana kamwe na tabia hii, maana nachafuliwa kwa
makusudi na kusababisha wapiga kura wangu wajenge chuki dhidi yangu,
alisema.
Kamanada wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabasi, alipoulizwa alisema:
“Mimi silijui suala hili, nimesikia katika vyombo vya habari,
ninachojua mimi risasi zilifyatuliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu,
Wilaya ya Arusha (NEC), Godfrey Mwalusamba wakati akimwokoa Mussa
Hamisi, aliyekatwa panga, wakati akimwokoa mama mmoja aliyedaiwa kugawa
pesa za kuhonga, wapiga kura wa Daraja Mbili ili kuipigia CCM,”alisema.
Alisema Mwalusamba alilazimika kufyatua risasi baada ya kumwona Mussa
Hamisi, akikatwa panga na kundi la watu hao walitawanyika na kuwa watu
wanane walitiwa mbaroni.
CHANZO: NIPASHE
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII