KAMA WEWE NI MWANA CHADEMA, HII INAKUHUSU SANA... PLEASE READ

CHADEMA: Viongozi wa mikoa na wilaya (Chadema) ambao wanashindwa kufanya kazi zao waondoke.
Chaguzi baada ya chaguzi, ipo mikoa tunaona jinsi inavyotamalaki
ushindi wa CDM kila chaguzi zinapofanyika, na zile ambazo zina bank kura
nzuri pamoja na kwamba tunashindwa na zile ambazo zinaonyesha kudorora
kwenye kila chaguzi.
Chama hiki cha siasa ni chama kinachokuwa kwa kasi kina hitaji viongozi
makini, wasomi, na wenye uwezo mkubwa wa kuona mambo, kupambanua na
kutenda. Natumaini viongozi wetu wa chama wa mikoa na wilaya, tarafa na
kata ni wale wenye weledi wa kuthubutu na kufikia viwango halisi vya
viongozi.
Uongozi unaonekana kwa kiwango cha kuweza kufikia malengo uliyopewa,
kiongozi wa kisiasa wa mkoa na wilaya ndio wana hakikisha ukuzi wa chama
ngazi husika wakishirikiana na viongozi wa kata na vijiji. Kuna haja ya
kufanya tathimini kama hawa viongozi wana fanya kazi zao ipasavyo.
haiwezekani wilaya nzima tukakosa hata kata moja kwa Udiwani au mkoa
mzima tukakosa ubunge.
Viongozi wanaotegemea mpaka viongozi wa taifa wafike ndio wafanye kazi
hawatufai. lazima chama kijikite na kujijenga ngazi ya kata, wilaya na
mkoa ili kuweza kuwafikia wengi kwa wakati muafaka.
Chaguzi zinatoa mwanga wa kukua kwa chama kwani kura zinaonyesha chama
kinakuwa, sasa umakini unahitajika zaidi kuliko wakati wowote. Hakuna wa
kulaumiwa 2015.
Imeandikwa na Chief Mkwawa wa kalenga (JF)
Hatukumshinda mkoloni kwa imani, bali kwa vitendo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII