Pages

Wednesday, October 31, 2012

'SIWEZI KUMSALITI VENGU'....... : STELLA


MISS Kinondoni 2009, Stella Mbuge amefunguka kuwa ugonjwa wa mpenzi wake Joseph Shamba ‘Vengu’, memba wa Orijino Komedi si sababu ya kumuacha na kuhangaika na wanaume wengine.


Akipiga stori na mtandao wa mpekuzi , Stella alisema, anatambua kuugua ni sehemu ya maisha na jambo kubwa kwa sasa ni kumuombea mpenzi wake huyo apone haraka na kuendelea na maisha yao kama kawaida.

 “Vengu ana thamani kubwa kwangu, siwezi kumuacha wala kumsaliti. Ndugu zake wananipenda na kunipa ushirikiano mzuri. Nashukuru anaendelea vizuri na ninaamini siku si nyingi atarudi kazini,” alisema Stella.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII