
Catwalk Professor akila pozi baada ya kushinda tuzo yake ya Beffta

Fabrice Muamba akiwa na furaha tele baada ya kukaribishwa kwa shangwe na shauku na wadau

Fashionista Mamaa Jestina George aka mama Iman ndani ya mambo ya Red Carpet

Frank Eyembe akila pozi na Fabrice Muamba

Frank akiwa na Actor Wale Ojo baada ya kunyakua tuzo ya best actor

Makamuzi yakiendelea

Msanii Nathan baada ya kumkabidhi tuzo mama yake

Mtangazaji
Nguli wa zamani wa ITV sir Trevor McDonald akisema machache baada ya
kupokea Tuzo ya Beffta ''LIFE TIME ACHIEVEMENT ''

Warembo waking'ara ndani ya red Carpet

kutoka Kulia Ceo wa Beffta Pauline Long akitaja washindi wa tuzo za mwaka 2012
Kwa picha zaidi bofya read more

kutoka kulia Mshindi wa best of Best Fashion Choreographer 2012 Yvonne, Jestina, Peace na Frank

sehemu ya kadamnasi ilivyofurika wadau kutoka sehemu mbalimbali

show zikiendela
Urban
Pulse na Miss Jestina blog wanakuleta taswira mbalimbali kutoka katika
tuzo za Nne Beffta 2012 zilizofanyika jumamosi tarehe 27 Octoba 2012
ndani ya Ukumbi wa HIPPODROME,GOLDERS GREEN, LONDON NW1 7RP. Tuzo hizi
ziliandaliwa maalum kwa ajili ya kutambua michango mbalimbali ya wasanii
na wataalam katika tasnia ya luninga, Filamu, Internet, Mitindo,
Magazeti, Majarida, Muziki,Tamthilia,Tovuti na Blogs, Kucheza, Mashairi,
na michango ya watu fulani mashuhuri katika kukuza au kuimarisha
jamii ya watu weusi hususani wafrika waishio hapa nchini Uingereza.
Mojawapo
ya tuzo za muhimu Beffta zilikwenda kwa mtangazaji nguli wa zamani wa
ITV Sir Trevor Mcdonald aliejinyakulia tuzo ya " Life time Achievement"
kutokana na mchango wake katika tasnia ya utangazaji.
Mbali
na hapo tuzo za Beffta zilienda maili zaidi kwa kumkaribisha mchezaji
wa zamani kutoka timu ya Bolton ambaye alifariki uwanjani kwa mda wa
dakika 54, lakini kutokana na nguvu pamoja na miujiza ya mwenyezi mungu
kwa kuwawezesha madaktari aliweza kufufuka na kuwa hai hadi leo hii.
Mchezaji huyu mwenye asili ya Kikongo aitwaye Fabrice Muamba alifunga
pingu za maisha hivi karibuni na mchumba wake Shauna Magunda pia ndio
aliekua mgeni rasmi katika sherehe hizi za tuzo za Beffta 2012.
Tuzo za Beffta zimeanzishwa miaka minne iliyopita na Pauline Long kutoka Kenya ambaye ndio CEO wa tuzo za Beffta.
Source: Urban Pulse and Miss Jestina Blog
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII