Pages

Friday, November 16, 2012

AGNES MASOGANGE AMUANIKA MPENZI WAKE BBM


VIDEO Queen, Agness Jelard ‘Masogange’ hivi karibuni ameamua kumuanika mpenzi wake aitwaye Evance Komu kupitia mtandao wa BBM.
 
Agness Jelard ‘Masogange’.
Masogange alifanya hivyo kwa kutundika picha zinazomuonesha akiwa kimahaba na mwanaume huyo kisha kusindikiza na maneno yasemayo; ‘mke wa Komu’.

Aidha, msanii huyo amemlalamikia mtu mmoja aliyejipachika jina la Agnes kisha kufungua akaunt kwenye facebook na kuweka picha zake na kuwatongoza wanaume.

“Nimechoshwa na huyu mtu, nikimbaini kweli nitamuumiza kwani ananishushia hadhi yangu, mimi nina wangu najiheshimu, siwezi kujiuza mtandaoni,” alisema Agness.

Evance alianza kupata umaarufu miaka kadhaa iliyopita baada ya kujitosa katika tasnia ya filamu Bongo ambapo alianza kucheza filamu ya Roho Sita na Valentine Day zilizosumbua sokoni.

SOURCE: GPL

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII