HIKI NDO ALICHOKISEMA KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA KUHUSU KIFO CHA SHARO MILLIONEA
Taarifa Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri
Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye
barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein
Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota
Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la
Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka
mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa
kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye
sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza
ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.Kwenye gari
alikua mwenyewe
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII