Pages

Monday, November 5, 2012

Homa ya uchaguzi wa Marekani yazidi kupanda wakati kampeni zikifikia ukingoni

Mahasimu wa kisiasa nchini Marekani ambao wanawania kiti cha uraisi,Mitty Romney na Barack Obama


Kampeni za lala salama nchini Marekani zimeendelea huku Rais Barack Obama na hasimu wake kisiasa Mitt Romney wakiendelea kujinadi kwa wananchi lengo likiwa ni kusaka kura ambazo zitawapeleka katika Ikulu ya White House.

Baada ya kampeni za miaka miwili nchini Marekani wananchi wa Taifa hilo wanatarajiwa kupigakura kesho tarehe sita kuamua nani atakuwa Raisi.
Kwa upande wake Romney ambaye ni kinara wa kukosoa sera za Rais Obama hakurudi nyuma kwenye harakati zake na badala yake akabainisha kwa wananchi kile ambacho kimeshindikana kwenye utawala wa Obama hususan akizungumzia changamoto ya ajira.
Wachambuzi wa Siasa wanaendelea kumpa nafasi Rais Obama kuweza kutetea wadhifa wake huku suala la kushughulikiwa kwa madhara ya kimbunga cha sandy likionekana kumuongezea sifa raisi Obama.
Wananchi wa Marekani wameshaanza kupiga kura mapema wengi wao wakiwa ni wanachama wa Chama Cha Democratic huku kura za Jopo zinazopigwa kutoka kila Jimbo ndizo ambazo zitaamua nani awe Rais.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII