CELINE Dion ni mwanamuziki wa Canada, ambaye ana jina kubwa katika
medani ya muziki akiamianika kuwa ndiye anayeshikilia rekodi ya kuuza
kazi nyingi zaidi za muziki.
Dion ambaye alianza shughuli za muziki akiwa na umri wa miaka mitano,
ana utajiri wa kiasi cha Dola 600 milioni (Sh 50 bilioni za Kenya).
Mkali huyo anasifika kwa sauti nzuri huku akiwa mahiri wa kuimba muziki wa taratibu, R&B na wakati mwingine classical.
Aliibuka zaidi mwaka 1990 wakati alipoachia albamu ya Unison na
kumfanya ajizolee sifa katika nchi za Marekani, Canada na nchi za
Jumuiya ya Madola.
Jina la Dion lilijulikana zaidi katika miaka ya 1980 baada ya
kushinda mashindano ya kuimba ya Yamaha World Popular Song Festival
mwaka 1982 na yale ya Eurovision baada ya kuiwakilisha Uswisi mwaka
1980.
Hata hivyo, wimbo wa 'My Heart Will Go On' uliotumika katika filamu
ya Titanic ndio uliompa chati zaidi katika medani ya muziki.
Dion anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke pekee, ambaye aliuza zaidi ya nakala milioni 200 duniani kote.
Mwanamuziki huyo ametengeneza utajiri wake kutokana na biashara ya
migawaha. Ana migawaha kadhaa nchini Canada iliyo chini ya kampuni yake
ya Nickel Restaurants.
Dion anamiliki jumba kubwa katika mji wa Montreal, Quebec ikiwa na thamani ya Dola 29 milioni (Sh 2.5 bilioni za Kenya).
Nyumba huyo ina vyumba sita vya kulala, sehemu ya chakula, jiko, maktaba, gym na sehemu ya kuogelea.
Pia jumba jingine nchini Ufaransa katika eneo la Montmorency kwenye
jiji la Paris likiwa na thamani ya Dola 47 milioni (Sh bilioni nne za
Kenya).
Anamiliki nyumba nyingine katika eneo la Notre-Dame De La Merci lililoko katika mji wa Quebec, Canada.
Dion anamiliki pia klabu ya Le Mirage, ambayo ina eneo kubwa la
kucheza mchezo wa gofu huko Quebec. Aliwekeza kiasi cha Dola 15 milioni
(Sh 1.4 bilioni za Kenya) katika klabu hiyo.
Dion anamiliki magari kadhaa lakini mojawapo aina ya Royal Royce Corniche, ambalo limebuniwa na Bill Allen.
Pia anamiliki ndege aina ya Bombardier, ambayo ina vikolombwezo
mbalimbali. Ndege kama hiyo wanayo matajiri Bill Gates na Steven
Spielberg.
The aircraft, operated by Vesey Air on behalf of owner Celine Dion |
Dion na Rene Angelil walikutana mwaka 1980 wakati Dion akiwa na umri
wa miaka 12. Walioana Aprili 17, 1994, katika kanisa la Notre-Dame
Basilica mjini Montreal, Quebec.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII