Pages

Tuesday, November 27, 2012

TAZAMA KAZI ZA MAREHEMU SHARO MILLIONEA KABLA UMAUTI HAUJAMFIKA



KOMEDIAN ambaye pia alikuwa msanii wa muziki wa Bongofleva, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefariki dunia leo majira ya saa mbili usiku katika ajali ya gari. Sharo amefikwa na mauti wakati akiwa safarini akitokea Dar es Salaam kuelekea nyumbani kwao, Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga. Msanii huyo alikuwa anaendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T478 BVR na amepata ajali eneo la Songa- Maguzoni wilaya ya Muheza mkoani Tanga. Marehemu alikuwa peke yake kwenye gari. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe amethibitisha kutokea ajali hiyo na katika taarifa yake kwa vyombo vya habari saa chache baada ya ajali,  alisema kuwa mchoro wa ajali unaonesha kuwa gari la marehemu liliacha njia kabla ya kupinduka mara kadhaa. Naye Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kubainisha kwamba gari alilopata nalo ajali limeharibika sana.

“Mimi sijafika eneo la tukio lakini nimezungumza na OCD wetu hapa Muheza, Andrew Satta yeye alifika eneo la tukio na kunipa taarifa kamili. Ukweli ni kwamba msiba huu ni majonzi na pigo kubwa kwa Wilaya ya Muheza kwa sababu huyu kijana ni mzawa wa hapa.
“Muheza tulikuwa tunajivunia kipaji cha Sharo Milionea lakini hatuna jinsi, kila kitu kinapangwa na Mwenyezi Mungu,” alisema Mgalu.














No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII