Mwakilishi wa Rwanda katika shindano la Miss East Africa 2012.
Mwakilishi wa Kenya katika shindano la Miss East Africa 2012.
Mrembo atakayeiwakilisha Rwanda ni UMWARI NEEMA (22) ambae
ana urefu wa futi 5.9 ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo
cha Kigali Institue of Education ( KIE) na pia ni mfanyakazi wa Kampuni
ya simu za mkononi ya Tigo jijini Kigali.
Mrembo atakaeiwakilisha Nchi ya Kenya ni JOAN WAMBUI NDICHO
(18) mwenye urefu wa futi 5.8 na anayetarajia kujiunga na Chuo kikuu
cha Machakos University College kusomea mambo ya utalii
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika
tarehe 07 mwezi December mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini
Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi,
Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu
yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye
luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa
Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na
kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII