Leo
asubuhi huko Msasani, Dar es Salaam, wadau TV na Filamu hapa nchini
walialikwa kushuhudia onyesho la kwanza la Tamthilia mpya iitwayo Siri
ya Mtungi. Tamthilia mpya hii ya kusisimua itatangazwa kila wiki siku ya
Jumampili saa 3:30 usiku kwa njia ya ITV na kurudiwa saa 3:30 usiku
jumaatanu ifuatayo kwa njia ya EATV.
Tamthilia
hii mypa imetekelezwa na JHU-CCP (John Hopkins Bloomberg School of
Public Health Center for Communication Programs); kwa msaada wa Watu wa
Marekani (USAID – United States Agency for International Development) na
PEPFAR (US President's Emergency Fund for AIDS Relief). Ikiwa
imetayarishwa na MFDI (Media for Development International) na inwaleta
pamoja Wasanii bora wa Tanzania, waandishi, wana mitindo
nguo,wakurugenzi wa sanaa, waigizaji na watendaji wa filamu kwenye
mafanikio makubwa ya ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni Tanzania.
Pia tamthilia hii ni kati ya juhudi za programu ya awali ya TCCP
(Tanzania Communication Capacity Project).
Katika
maonyesho hayo, huko Msasani, wadau walikaribishwa na kupata fursah ya
kuonana na waundaji, waandishi, waigizanji na watekelezaji wengine wa
tamthilia hiyo. Pia walipata fursah ya kuhudhuria studio hiyo na kuona
waigizaji wakiigiza kipande kidogo cha tamthilia hiyo pale pale studio
akiwemo muigizaji mahiri hapa mjini wa Monalisa!
Kwa habari zaidi kuhusu Siri ya Mtungi jiunge na kurasa wao wa Facebook (www.facebook.com/SiriyaMtungi) au fuatilia mtiriko wa uhondo huko Twitter kwa kujiunga na @SiriyaMtungi (http://www.twitter.com/SiriyaMtungi). Pia chukuwa fursah kupitia tovuti ya tamthilia (www.siriyamtungi.com
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII