FLAVIAN MATATA ATWAA TUZO YA MWANAMITINDO BORA WA AFRICA....SOMA ZAIDI HAPA
MWANAMITINDO
wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ambaye ameng’ara kimataifa
baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa
mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding
Model 2012).
MWANAMITINDO
wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara kimataifa
baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa
mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding
Model 2012).
Tuzo hiyo
utolewa kwa wanamitindo ambao bado wanailetea sifa Afrika kimataifa na
Flaviana amekuwa katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba, Flaviana
alishinda tuzo nyingine ya uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya
Waafrika.
Flaviana
kwa ambaye kwa sasa anaishi na kufanya kazi ya uanamitindo New York
nchini Marekani kupitia shirika la Wilhelmina Models, mpaka sasa ameweza
kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho
ya mavazi.
Tangu
ashinde taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana amekuwa
aking’ara katika kona zote za dunia na hasa baada ya kumaliza katika
nafasi ya sita katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, huku
Tanzania ikishiriki kwa mara ya kwanza.
Ameweza
kushiriki katika maonyesho ya mavaz mengi Ulaya na Amerika huku akitoa
misaada mingi kwa Watanzania wenzake ambao wamekuwa na ndoto ya kufika
mbali katika fani hiyo.
Kwa sasa
Flaviana anaendesha taasisi yake, Flaviana Matata Foundation ambayo
inasomesha watoto wa kike 16 na mwaka jana alitoa msaada wa vifaa vya
kuokoa maisha kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba
huku ikiwa kumbukumbu ya kifo cha mama yake mzazi katika ajali hiyo ya
mwaka 1996.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria
Sarungi Tsehai alisema kuwa wamejisikia faraja sana kwa kumvumbua
mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa anashika chati ya juu Tanzania na nje
ya nchi.
Maria
alisema kuwa Flaviana amedhihirisha ubora wake na mpaka sasa amepitiliza
kiwango cha kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, ndoto ambayo
alikuwa nayo muda mrefu.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII