Pages

Monday, January 28, 2013

JOKATE, KADINDA KASHFA NZITO YA KUHUSIKA KUANZISHA DANGURO SOUTH AFRIKA


WANAMITINDO maarufu Bongo, Jokate Mwegelo na Martin Kadinda, wamekanyaga kashfa nzito baada ya kuhusishwa na umiliki wa danguro la wasichana nchini Safrika Kusini ‘Sauzi’, Ijumaa Wikienda limetonywa.
 
Jokate Mwegelo.
Akizungumza na GPL, msichana aliyejitambulisha kwa jina la Hilda Andrew alisema kuwa alikumbana na mkasa mzito baada ya kuchati na mrembo aliyejitaja kwa jina la Jokate na kumwambia kwamba anataka kumuunganisha kuwa mmoja wa wanamitindo wake nchini Afrika Kusini.

Msichana huyo alitiririka kuwa alikuwa akichati mara kwa mara na mwanadada huyo akijua ni Jokate hadi  wakawa wanapigiana simu huku akimwambia kuwa yuko Sauzi akiwaandaa wanamitindo aliowapeleka kwa ajili ya onesho lililokuwa likifanyika nchini humo.
Aliendelea kutambaa na mistari kuwa baadaye mwanamke huyo alimwambia amemuachia maagizo Martin Kadinda ambaye angemuona na kumpima nguo kwa ajili ya kwenda nazo kwenye maonesho Sauzi lakini cha ajabu siku ya kukutana na Martin Kadinda alikuja kaka mwingine na kumwambia kuwa ametumwa na mwanamitindo huyo kwa vile alikuwa ana kazi nyingine nyingi.

Martin Kadinda.
Hilda alisema kuwa waliendelea kuzungumza na mwisho walifikia uamuzi wa kwenda bondeni kwa Mzee Madiba na kwa kuwa alikuwa na ‘pasipoti’, haikuwa shida na alipofika uwanja wa ndege alipokelewa vizuri na kupelekwa sehemu ambayo kulikuwa na wasichana wengi bila kuwaona Jokate na Martin Kadinda ndipo nikagundua mchezo mchafu, nikaamua kufungasha virago vyangu na kurejea nyumbani.
Baada ya kupata madai hayo, gazeti hili lilimtafuta Martin Kadinda ambaye alikiri kusikia ishu hiyo na kusema kuwa hata yeye inamuumiza kwani ni  watu tu wanatumia majina yao kuwachafua hadi hivi sasa mambo yake mengine yamekwama kwa ajili ya watu hao.
Kwa upande wake Jokate alisema kuwa anaumizwa na watu wanaotumia jina lake kumchafu kiasi hicho na kuwasihi akina dada kuepukana kuchati na watu wasiowajua

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII