SERIKALIya Uswisi imesema Serikali Tanzania haijaonyesha nia ya dhati kutaka kuchunguzana kupata mabilioni ya fedha yaliyofichwa na Watanzania katika benki mbalimbalinchini humo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Gazeti la Mwananchi Jumamosi, jijini Dar esSalaam jana, Balozi wa Uswisi nchini, Olivier Chave alisema mpaka sasa hakunajitihada zozote zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kutaka ufumbuzi wa tuhumahizo.
Balozi Chave alisema hayo muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yake yaMbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. Hata hivyo wote wawili hawakuwa tayarikueleza ni kipi kilichojiri katika mazungumzo yao.
Katika kikao cha tisa cha Bunge, Novemba mwaka jana, Zitto aliwasilisha hojabinafsi kulitaka Bunge kuchunguza na kuielekeza Serikali kuchukua hatua dhidiya Watanzania walioficha fedha na mali haramu nje ya nchi.
Katika mazungumzo yake jana, Chave alisema: “Uswisi iko tayari kushirikiana naTanzania kujua uhalali wa fedha hizo na endapo zikigundulika ni fedha chafubasi tutazirejesha nchini.” Aliongeza:
“Serikaliya Uswisi haina tatizo kwani tumeshafanya hivyo kwa nchi za Ufilipino naNigeria hivyo tutafurahi na Tanzania kama tutamaliza suala hili”.
Alisemahabari zinazoandikwa kuhusu mabilioni hayo kuhifadhiwa katika Benki za Uswisi,zinaharibu picha ya nchi hiyo mbele ya mataifa mengine, hivyo angependa sualahilo kumalizwa na kwamba wao wako tayari kusaidia.
Kauli ya Zitto
Kwa upande wake, Zitto alisema hadi sasa Serikali haijamfuata kutaka kutoaushirikiano wa aina yoyote kuhusu tuhuma hizo.
Alisema kuwa ingawa Serikali ilitaka iachiwe tuhuma hizo ili iweze kuzifanyiakazi, lakini hadi sasa ukimya umetawala.
“Tangu kuahirishwa kwa kikao cha Bunge sijafuatwa na AG (Mwanasheria Mkuu waSerikali) wala mtu yeyote na sijui kipi kinachoendelea,” alisema Zitto nakuongeza:
“Nitaandika barua na kumkabidhi AG siku ya Jumatatu (keshokutwa ), nitahojinini kinachoendelea katika uchunguzi huo.”
Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Naibu Katibu MkuuChadema, alisema Serikali ya Tanzania haionyeshi nia ya kuzihitaji fedha hizo.Aliongeza kwamba kuna njia mbili za kuwabaini walioficha mabilioni hayo nchiniUswisi. Kwanza ni kwa Serikali ya Tanzania kushirikiana na Serikali ya Uswisi,pili ni ulipaji wa kodi wa fedha ambazo Watanzania wameweka katika benki nchinihumo.
“Njia hii ya pili nayo ni rahisi kwa sababu ukienda kuuliza Uswisi wanaolipiafedha hizo utapata majina yao. Hivyo Serikali itaweza kukamilisha taarifa yakena kuiwasilisha bungeni katika kikao kijacho” alisema Zitto.
Taarifa kutoka Benki Kuu ya Uswisi inaonyesha kuwa baadhi ya fedha hizozimewekwa katika akaunti za vigogo hao na kampuni za mafuta na gesi zilizoponchini.
SOURCE: MCL
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII