Pages

Thursday, January 24, 2013

PICHA NA VIDEO YA MAANDAMANO YA WANACHUO WA ST.JOHN'S KUPINGA VITENDO VYA UBAKAJI VINAVYOENDALEA KUWAKUMBA


Wanafunzi wakiwa na mabango leo mjini dodoma.
ZAIDI ya wanafunzi 4000 wa Chuo Kikuu cha St. John’s kilichopo mjini DODOMA  wameandamana wakililalamikia Jeshi la Polisi Nchini kwa kushindwa kuthibiti vitendo vya matukio ya ubakaji na kulawitiwa yanayofanyika chuoni hapo.

Wanafunzi hao ambao waliandamana umbali wa kilomita tatu leo kutoka chuo kilipo na kuishia viwanja vya Mwalimu Nyerere walidai wanalenga kufikisha ujumbe kwa jamii kutambua vitendo vya kikatili vinavyofanyika chuoni hapo.
Maandamano hayo ambayo yalikuwa yakisindikizwa na
Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia, yalipita katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma.

Waandamanaji hao ambao mbali na kuimba nyimbo za kulilaumu Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuthibiti vitendo hivyo, pia mabango waliyokuwa wamebeba yalikuwa yakililaumu jeshi hilo.
Askari jeshi la polisi wakijariobu kuwazuia wanafunzi leo mjini dodoma

Huyu jamaa alielala chini ni mtuhumiwa aliekamatwa asubuhi ya leo, ambapo wanafunzi walivamiwa na kuibiwa Laptop kisha wavamizi hao kuchoropoka. Wanafunzi ilibidi wajikusanye muda huo huo na kuwasaka ndipo walipokutana na jamaa huyo ambae alikuwa haeleweki na baadae ikafahamika ni mmoja wao

Basi mtuhumiwa huyo alichukuliwa na polisi kisha wanafunzi waliingia chuoni kuanzisha maandamano

Hapa walikusanyika kwenye bendera kisha kuongea na mkuu wa chuo

Mkuu wa chuo alisema pia nao wamechoshwa na mambo mabaya ambayo wanafunzi wanafanyiwa. Hivyo wanafunzi wawe na subira wanafanya taratibu za kibari cha maandamano ya amani

Wanafunzi baada ya kusubili kwa muda mrefu kibari icho wakaamua kuandaa mabango kwa ajili ya maandamano, ambapo kibari kipatikane kisipatikane walidai kuandamana ni lazima
Basi wanafunzi wakaanza kuchora mabango yao kwa ajili ya maandamano



Mabango yalipokamilika wakasimama kwenye bendera kwa mara nyingine



Walifika mbali na kuona kuwa polisi wanahusika katika mambo mabaya wanayofanyiwa. Ndipo wakachora bango hili kuonyesha hisia zao
Wakaamua kuingia barabarani kwa maandamano baada ya kujaa munkari na jaziba kubwa
Hapa wapo barabarani na masomo kwa siku ya leo hayakuwepo

Bango lina picha ya mwanafunzi alieuliwa kikatili, aliefahamika kwa jina la LYDIA LEO




Ni mchaka mchaka ulioendana na nyimbo za hisia

Magari yalisimama kwa muda mrefu mjini hapo mpaka wanafunzi walipomalizika kupita, kwa hiyo wenye haraka walichelewa

Haya huyu anaashiria demokrasia na maendelea ndio imetawala juu yao

Msafara hapa unaelekea maeneo ya Bungeni

Kila walipopita walikuwa wakishindikizwa na polisi kuhakikisha amani inatawala

Hakuna kitu ambacho kiliniacha hoi baada ya wanafunzi kwenda mpaka Bungeni, kisha walipofika wakaimba nyimbo ya Taifa. Polisi waliwaomba kuongea na viongozi wa maandamano hayo wakajibiwa na wanafunzi kuwa kiongozi wao hameishakufa ambae ni mama LYDIA LEO

Gari la maji ya kuwasha lilikuwepo lakini wanafunzi hao hawakutishika na kitu chochote kile kutoka kwa Polisi

Wanafunzi walifika mpaka Nyerere Square waliimba nyimbo mbalimbali mahala hapo




Baada ya kutembea mji mzima na mabango yao na kuhakikisha kiu yao imekwisha basi waliamua kurudi chuoni

Gari la washa washa nalo lilikuwepo lakini watu walikuwa na jaziba zao vilevile mwanzo mwisho
Add caption
Barabara zilikuwa zimetawaliwa na wanafunzi kwa kiasi kikubwa, mpaka kusababisha magari kutopita

Hapa ilibidi nipande gari la polisi ili niweze kuchukua picha vizuri, sio siri polisi wenyewe walikuwa wamechoka kwa kutembezwa mji mzima baada kuchat nao kwenye gari ilo

Hapa ndipo safari ya maandamano ilipoanzia na ndipo safari hiyo ilipoishia maeneo haya ya kwenye bendera mbele ya jengo la administration.

Safari ya maandamano ya amani ikawa imeishia chuoni hapo baada ya kuona kuwa ujumbe wao umefika. Wanafunzi wa chuo wamechoshwa na matendo mabaya ambayo wanafanyiwa ikiwa ni pamoja na kubakwa, kulawitiwa, kuibiwa vitu vyao kama Laptop na vitu vingine. Wameonesha umoja wao kwa sababu ya kuchoshwa na mambo hayo, ambapo leo asubuhi kuna wanafunzi walivamiwa na kuibiwa Laptop. Hivyo wakaamua kujikusanya asubuhi hiyo hiyo mida ya saa kumi na mbili alfajili na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye walimpiga na baadae kuchukuliwa na polisi.
TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILI PIA HAPA

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII