Pages

Thursday, January 24, 2013

PINDA ATOA MAONI KUHUSU KATIBA MPYA, APENDEKEZA MADARAKA YA RAIS YAPUNGUZWE....SOMA ZAIDI HAPA



WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amependekeza katika Katiba mpya ijayo, madaraka ya Rais
yapunguzwe hasa katika shughuli za uteuzi wa viongozi.

Akizungumza jana baada ya kutoa maoni mbele ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Pinda alisema muda aliokaamadarakani na Rais Jakaya Kikwete, ameona ana mambo mengi na ndiyo maana anapendekeza si lazima kila jambo liende kwake. “Ni vema machache yabaki kwake. Kwa mfano uteuzi wa nafasi mbalimbali vipewe vyombo vya kufanya uteuzi huo,” alisema bila kufafanua nafasi ambazo Rais anatakiwa kuacha kuteua. Kuhusu nafasi ya Waziri Mkuu, alisema hiyo ni ya utendaji na kwa sasa Waziri Mkuu lazima awe mbunge na kutokana na hali hiyo, anapendekeza itazamwevizuri.
Alifafanua kuwa Waziri Mkuu atajikuta akilazimika kuangaliazaidi Serikali huku jimbo
analowakilisha likilala kwa kukosa usimamizi mzuri.Kutokana na hali hiyo, alipendekeza mawaziri
wasitokane na wabunge, ili wafanye kazi vizuri ya kusimamia majimbo yaowakisaidiana na  wananchi. Uhuru wa Bunge, Mahakama Alisema Bunge na Mahakama ni vyombo muhimu vinavyostahili kupewa nafasi ya kutosha.

Alizungumzia mifuko iliyoundwa ya Bunge na Mahakama na kutaka itambuliwe kikatiba na Katiba
ielekeze ni namna gani itumike. Kuhusu kinga ya mbunge, alisema ni vizuri itamkwe kwenye Katiba kuwa mbunge ana kinga, lakini ibaki bungeni tu si azungumze nje na kinga ya Bunge iendelee
kumlinda.
Akizungumzia Muungano, Pinda alisema tangu azaliwe hadi anapata akili mwaka 1964, alikuta Muungano na ndicho kitu pekee anachoweza kukisemea vizuri kwa kuwa
umejenga udugu, muungano na ukaribu.
“Hapakuwa na huyu ni mgeni,au huyu ametoka huku aukule,” alisema akizungumzia Muungano wa Serikali mbili ulivyo. Alikiri kuwa kuna kero nyingi za Muungano na kupendekeza kuwa dawa ya kero hizo si kuua Muungano, bali kitafutwe chombo kitakachoshughulikia
matatizo.
Alipendekeza Serikali zibaki mbili lakini iundwe tume ya kushughulikia matatizoyaliyopo. Pia  akapendekeza kuundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa Tanzania Bara kama ilivyo Zanzibar na vyama
vyote vipate ushiriki. Mafuta, gesi Akizungumzia rasilimali za Taifa za mafuta na gesi, Pinda
alisema haoni shida mafuta kuchimbwa Zanzibar na kusafirishwa Bara au kuchimbwa Bara na kusafirishwa Zanzibar kwa kuwa atavuka tu kununua na kurudi.
Chanzo: Habari leo.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII