STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, aliyekuwa mke wa marehemu
Juma Kilowoko ‘Sajuki’, amewaomba Watanzania wakiwemo wasanii wenzake
kuacha kuongea mambo mengi kwenye magazeti ikiwa ni pamoja na lawama na
kwamba dua kwa marehemu ndiyo jambo la msingi kwa sasa.
Akizungumza na Gazeti la Ijumaa hivi karibuni, Wastara alisema watu wanaongea
mengi na wataongea mengi kuhusu marehemu mume wake ikiwa ni pamoja na
lawama za nani amesababisha kifo, nani hajasababisha lakini akasema
waachane kabisa na mambo hayo kwani aliyeumia sana ni yeye.
“Ukweli utabaki kuwa Sajuki ameondoka kwa mipango ya Mungu, tuache lawama zisizo na msingi, tumuombee mwenzetu huko aliko apumzike kwa amani lakini waniombee pia niweze kuvuka kipindi hiki kigumu,” alisema Wastara.

No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII