Nimeidaka hii nikaona niwashirikishe sehemu ya maandiko ya Zitto:
Unaweza kuendelea kusoma kwa kirefu hapa - Mtwara: Serikali inavunja nchi kwa kutosikiliza Wananchi! | Fikra Pevu
Kwa udhaifu wa serikali na tabia ya kutafuta mchawi badala ya
kutatua tatizo la msingi, wananchi wameendelea kukutana na hata wengine
sasa kuanza kusambaza ujumbe wa kukata kipande cha nchi na kuanzisha
Jamhuri ya Kusini. Nimeona kwenye mabango ya mkutano wa hadhara
uliofanyika 19/1/2013 wananchi wakibeba mabango yanayoaishiria kuchoka
kuwa sehemu ya Tanzania na kuanzisha Jamhuri ya Makonde kuanzia jiwe la
Mzungu wilayani Kilwa mpaka mto Ruvuma. Haya yanatoka na kiburi cha
Serikali kujishusha na kuwasikiliza wananchi wanaodai haki yao ya
kikatiba.
Ni Serikali iliyokosa uhalali wa kutawala inayoweza kudharau hisia hizi za wananchi. Serikali ielewe kwamba kamwe haitaweza kulinda kila nchi ya bomba hili iwapo italijenga kwa nguvu. Badala ya kuzungumza na vyombo vya habari Serikali ifanye mazungumzo na wananchi wa Mtwara na kukubaliana na matakwa yao. Kitendo cha Serikali kung’ang’ania msimamo wake dhidi ya watu wa Mtwara ni kitendo kinachoweza kuipasua nchi na hivyo kwenda kinyume na masharti ya katiba ibara ya 28 ambayo inasema: “Kila raia ana wajibu wa kulinda uhuru wa nchi, uhuru mamlaka na umoja wa taifa.” (Ibara ya 28, 1)
Inawezekana Serikali inaogopa kuvunja makubaliano na Wachina ya mkopo wa dola za kimarekani 1.2 bilioni ambao imeuingia bila hata kushirikisha Bunge. Inawezekana pia Serikali na hasa watendaji wa Serikali waliojadili mkopo huu ‘wameshapata chao’ na hivyo kuogopa kusikiliza madai halali ya wananchi. Lakini yote hayo hayawezi kuwa zaidi ya Umoja wa nchi yetu. Hatuwezi kukubali nchi yetu ipasuke vipande vipande kwa sababu tu ya kulinda mkataba wa bilioni 1.2 tuliokopa China, ambayo serikali inang’ang’ania.
Tunafahamu kwamba ubalozi wa China umeandika barua serikalini kuwaondoa raia wa China waliopo Mtwara kwa hofu ya maisha yao. Serikali inaficha ukweli huu kama ilivyoficha ukweli kwamba Naibu Waziri wa Nishati na Madini bwana George Simbachawene alifukuzwa na wananchi wa Mtwara alipokwenda hivi majuzi. Serikali itaficha ukweli mpaka lini? Lazima tupate majawabu!
Kwanza Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa Bomba hili. Kamati ya Bunge ya POAC ilipokuwa inapitia mahesabu ya TPDC iliomba mkataba na kwa mshangao mkubwa wabunge wakaambiwa Mkataba haupo TPDC bali upo Wizarani! Kwanini Mkataba huu wa matrilioni ya Fedha unafichwa? Mkataba huu ulisainiwa pamoja mikataba mingine miwili, mmoja wa kujenga nyumba za wanajeshi wa thamani ya dola za kimarekani 400 milioni na mwingine wa mawasiliano jeshini wa dola za kimarekani 110 milioni, na mikataba yote mitatu imesainiwa kimya kimya bila kushirikisha wananchi kupitia Bunge. Lazima mikataba yote hii iwekwe wazi!
Pili, Mkataba huu uchunguzwe kama unalingana na thamani ya fedha maana kwa utafiti wa awali inaonyesha kuwa bei ya ujenzi wa bomba imepandishwa maradufu. Wastani wa kujenga bomba la gesi duniani ni dola za kimarekani 1.2 milioni kwa maili moja. Mradi huu wa Tanzania utagharimu dola za kimarekani 2.2 milioni kwa kilomita moja (maili 1 ni sawa na kilomita 1.6).

No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII