Hizb-ut Tahrir: KWANINI UISLAMU UNYONGWE KWA KITANZI KWA KISINGIZIO CHA MAUWAJI YA PADRI ?

images
Kumb: 06/1434 AH                      10 Rabi-ul Thani 1434 AH          20/02/2013 CE TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KWANINI UISLAMU UNYONGWE KWA KITANZI KWA KISINGIZIO CHA MAUWAJI YA PADRI ?

    
Kufuatia mauwaji ya kupigwa risasi kwa Padri wa Kanisa Katoliki  Evaristus Mushi, padri dhamana wa kanisa la St. Joseph Zanzibar yaliyotokea siku ya jumapili asubuhi, sisi Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki tunapenda kufafanua  yafuatayo: Kwa bahati mbaya sana tukio hili limekuwa kana kwamba lilikuwa likisubiriwa na wanasiasa pamoja na viongozi wa kikiristo kwa lengo la kutoa msukumo zaidi wa ajenda ya kilimwengu ya chuki na uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu. Kwa upande wa wanasiasa, kwa hakika ni fedheha kubwa isiyomithilika kwamba, badala ya kulikabili suala la kushindwa kulinda  maisha ya raia na mali zao tahamaki baadhi yao wamerukia  kuhitimisha kwamba tukio hili ni ‘tukio la ugaidi’.  Kauli hii ni jaribio la kutengeza ufahamu jumla (public opinion) wa kuuhusisha Uislamu na Waislamu moja kwa moja na tukio hilo. Ilhali wanasisa wanaepuka na kujisahaulisha kwa makusudi ukweli kwamba tukio hili lilitokea asubuhi kweupee! na karibu mno na Kituo kidogo cha Polisi. Pia wanaepuka ukweli wa kushindwa kwao kukabiliana na mfumo wa kiuchumi wa kibepari ambao unakuza pengo la kipato baina ya maskini na matajiri.Kitu kinachopelekea raia kuwa katika hali ya kukata tamaa, kutoaminiana  na  kuzusha uadui baina yao.
Amma kuhusiana na viongozi wa kanisa, badala ya kuukabili Uislamu kwa mjadala wa kimfumo wanaficha udhaifu wao kwa kudandia tukio hili nao pia kuchochea zaidi chuki na uadui wa kilimwengu unaosukumwa na mataifa ya Magharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu, vile vile wanafanya mbinu ya kuushawishi uchunguzi  wa tukio hili uwe na maslahi upande wao na mabwana wao wa kisiasa. Aidha, tukio hili linathibitisha tena kuwepo saratani iliyokita mizizi ndani ya Tanzania ya kuwapendelea Wakiristo, kwa kuwa tukio hili moja tu limeinua juu hisia ya serikali kiasi cha kuleta wachunguzi kutoka nje. Ilhali upande wa pili wanaharakati wa Kiislamu bado wanaendelea kusota korokoroni bila ya dhamana, na serikali inaonekana haijali wala kusikia kilio  chao.
Pia, Hizb ut -Tahrir tunapenda kuweka bayana kwamba kuuwa wachungaji na viongozi wa kidini, kuchoma moto majumba ya ibada na makanisa ni jambo lisiloruhusiwa ndani ya Uislamu. Na ni ukweli unaojuulikana na kila mtu namna dola ya Kiislamu ya Khilafah huko nyuma ilivyowatizama kwa uadilifu wasiokuwa waislamu, kiasi kwamba mpaka leo wanaendelea kuwepo katika nchi kubwa za kiislamu ambazo  idadi ya Waislamu ni kubwa zaidi.
Mwisho, tunatoa mwito kwa walio makini na waadilifu katika wakiristo kuingia ndani ya Uislamu. Na ikiwa hawajawa tayari, basi wajitenge mbali na mitego ya makafiri wa madola ya Magharibi hususan Marekani ambao wana kampeni ya uadui isiyomalizika dhidi ya Waislamu na Uislamu. Tunawaeleza wakiristo kwamba: Marekani ni dola ambayo daima hukandamiza nchi ndogo, kupora rasilmali zake na kuleta mtafaruku na migongano baina ya raia. Aidha, tunawakumbusha wakiristo na wasiokuwa Waislamu kwa jumla kwamba, hapana shaka yoyote  Uislamu utatawala tena dunia na utawatunza wote katika hali ya uadilifu na insafu kama ulivyowahi huko nyuma. Katika mwaka wa 638 AD wakati Padri Sophrinius wa Palestina alipolisalimisha eneo  la ardhi hiyo chini ya dola ya Kiislamu  ya Khilafah, khalifah Umar ra. aliandika waraka maalum kwa watu wa Aelia unaosomeka:
KWA JINA LA ALLAH, ARRAHMAN, ARRAHIYM
Huu ni Waraka wa mkataba kutoka kwa Umar  Mtumwa wa Allah, Amiri wa Waislamu, kwa watu wa Aelia. Anachukuwa dhamana ya usalama wa maisha yao, mali zao, makanisa yao namisalaba yao… Makanisa yao yasivunjwe wala yasiondoshwe, na kisiondoshwe chochote katika vitu vyao. Wasilazimishwe katika mambo ya dini, na wala asidhuriwe yoyote.
Ikiwa huo ndio uadilifu wa Uislamu kwa wasiokuwa Waislamu, basi hali itakuwaje lau watu hao wataingia ndani ya  Uislamu ? Muda umeshafika kwa wao kuchukuwa fursa hii adhimu ya kuingia ndani ya Uislamu  mara moja.
…………………. Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki
Tel +255 778 870609
Pepe:  jukwalakhilafah@gmail.com
Tovuti  Rasmi ya Hizb ut- Tahrir www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari  www.hizb-ut-tahrir.info
Source: wavuti.com
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

2 comments:

  1. kwani kusema kuwa tukio hili ni la kigaidi ndo kuuhusiha na waislam? kama kusema tukio hili ni la kigaidi ni kuusisha uislam kwa hiyo anataka kusema kuwa uislam na ugaidi ni kitu kimoja?

    ReplyDelete
  2. Islam means peace,have nothing to do with any violence committed by people

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs