Taarifa
zinasema kuwa,hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye mitambo ya
mawasiliano iliyopo katika chumba cha 11, kilichopo juu, mwisho kabisa
mwa jengo la minara ya PPF lililopo kwenye makutano ya Ohio/Garden
Avenue, katikati ya jiji la Dar es Salaam ndiyo iliyosababisha
moto asubuhi ya leo majira ya saa moja, na kusababisha jengo
hilo ushika moto.
Imetaarifiwa kuwa walinzi wa jengo hilo walishuhudia moshi mzito ukitoka ndani ya jengo hilo la ghorofa, ndipo walipotoa taarifa kwa vikosi vya zima-moto.
Kikosi cha uokozi kilifika kwa wakati katika eneo husika na pamoja na kuweko nyenzo katika jengo hilo za kukwea hadi ghorofa ya kumi na moja, ufupi wa mipira ya zima-moto ili kufikisha maji kwenye chumba kinachowaka moto ulikwamisha jitihada za kuuzima moto huo.

Hata na hivyo, juhudi
zilizofanywa na kikosi hicho zimefanikiwa kuuzima moto huo kabisa
mnamo mwendo wa saa tano kasoro za adhuhuri.
Polisi wapo katika eneo hilo ili kulinda mali zisiporwe au kuharibiwa na vibaka.
Hakuna madhara yoyote ya moja kwa moja kwa binadamu yaliyoripotiwa. Thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo nayo haijafahamika.

SOURCE: MPEKUZI
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII