Leo ndo yalikuwa ni mazishi ya Padri Evaristus Mushi aliyepigwa risasi akiwa katika
utekelezaji wa majukumu yake na hivi sasa ndo kuaga na kufanya misa ya
marehemu. Watu wengi mno na viongozi wa serikali,siasa na dini ya
kikristo wamehudhuria. Baadhi ni rais wa zanzibar Dr. Shein, Dr.
Slaa,mchungaji Mtikila. Walipotakiwa kueleza wameguswa vipi na kifo cha
padri.
Dr slaa amesema ni tukio la kusikitisha kutokea zanzibar kwani znz ndo
chimbuko la ukristo kwa Tz. Wamisionari wa kwanza walianzia znz.
Ameshangaa haya matukio yanajitokeza siku hizi. Tukio hili halina
maelezo ya kina kuhusu chanzo chake. Amesisitiza kuwa tusingependa kifo
cha aina hii kitokee kwa mtu yeyote na akasema muda umefika sasa
tujadili mizizi ya tatizo na si matawi na matunda ya tatizo.
Naye Mchungaji Mtikila amesema ni muda wa kutafakari,kuonyesha uvumilivu
kwa watanzania wote bara na visiwani. Amesema ni kipindi cha kutafakari
vitabu vitakatifu vinasema nini. Kwa waislam,amesema korani inasema
adui wao si wakristo bali ni mayahudi na makafiri.
Source: Radio Maria
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII