WARAKA KWA WATANZANIA : "MAAJABU, MAAJABU, MAAJABU X 20"
Imeandikwa na Omwilili Tayebwa, UDSM
Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi.Vivutio gani hivyo,?Ni
vivutio vya utalii.Watalii wengi wa ndani na nje ya nchi,wanapenda sana
,tena kutoka kwenye vitako vya mioyo yao,kushuhudia jinsi dhana ya
ujinga inavyoandaliwa ,kutengenezwa hatimae kupakuliwa kama
chakula.Matokeo ya kidato cha nne,mwaka wa masomo 2012/2013, yamefanya
watalii waongezeke ghafla nchini humu. Fuatilia rekodi za watalii
walioingia tokea tarehe kumi na saba hadi leo mwezi huu.Tatizo la
kushindwa kwa wadogo wetu si kwa sababu yao katika asilimia
kubwa. Serikali yetu chini ya Chama tawala mnachokijua, inapungukiwa
yafuatayo: AIBU,HOFU YA MUNGU,HURUMA NA AKILI TEKELEVU(Practiacal
intelligency). Mwaka huu ni wa pekee kweli. Halii hii imekuwa ikitokea
huko nyuma lakini si kwa furaha na vifijo kama mwaka huu!. Hata wanyama
wengine yaani hayawani wamenotisi jambo hili.Hivi simba na twiga
wasiodhuriwa na risasi wakichana mbuga kwa kukasirikia jambo
hili,tutakimbilia wapi ili tunusuru roho zetu. Ndugu zangu , KUNA MAANA
YOYOTE YA KUENDELEA KUIMBA WIMBO WA TANZANIA
NAKUPENDA,nakupeeeeendaaaaaaaaaaa!
Ni uwenda wazimuuuu!!!!Usiasa
umefunika utekelezaji.Zaidi ya nusu ya watainiwa,wamezungusha(MAANA YAKE
WANA SIFURI AU ZERO KWA KIINGEREZA)!!!!Eheheeeeeeeeheeee!!!! Utasikia
mipango mizuri serikalini ya kupeleka miradi ya maendeleo katika sehemu
fulafulani nchini, TANGU LINI MTU HASIYE NA ELIMU MBADALA AHUSISHWE
KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI AU MRADI HUO? UKWELI NI KWAMBA, FEDHA
ZIKITENGWA KWA MIRADI HIYO, HIZO NI KWA AJILI YA WAHUSIKA WALIOTUMWA NA
SERIKALI , WASIO NA HAYA WAENDE WAZITAFUNE. INAMAANARAIA WAKIPATA
ELIMU, DILI LITAVUNJIKA NA UFISADI UNANYIMWA NJIA, KWANI UFISADI NI
MOJAWAPO YA VYANZO VIKUU VYA KUKUSANYA PASIPO KUTAWANYA KWA BAADHI YA
VIONGOZI KTK NJE NA NDANI YA SERIKALI!! . JIULIZE,KUSHINDWA KWA WANAFUNZI
KWA KUSHANGAZA ,KUMEANZA LEO? KWANINI HAKUNA MSHTUKO NA UTEKELEZAJI
CHANYA KUTOKA SERIKALINI,KWANI NDIYO YENYE KUPANGA BAJETI?. IMEJIKITA
KATIKA USIASA BADALA YA VITENDO CHANYA.EBU ONJA YATOKEOAYO BUNGENI,KAMA
SEHEMU YA SERIKALI , KIDOGO .
KAMBI YA UPINZANI BUNGENI IKIFURUKUTA,CHAMA
TAWALA KINATOA TAARIFA YA UONGO,KURA ZA MIKONO ZINAAMRIWA NA ANA
MAKINDA,WENGI WAPE NDO LINAKUWA SULUHISHO LA MGOGORO.Hata mbuzi hawawezi
kuendesha BUNGE LAO,kwa namna hii!!!. KAMA NDUGU YANGU ULIFUATILIA
MVUTANO WA UWEPO WA CURRICULUM YA ELIMU HAPA NCHINI,HUKO BUNGENI,HUTAONA
TOFAUTI KWA MTIRIRIKO WA WARAKA WANGU,KAMA UNA UWEZO WA KUPAMBANUA NA
HUCHUKII UKWELI.Ningeishauri serikali la kufanya, ila sijui kama ina
blogi inayokusanya na kuheshimu mawazo ya raia wake.Serikali yetu ina
imani kwamba raia wake ni wajinga na imeisha jenga dhana ya
dharau. Bahati mbaya, si hivyo,ililenga kutumia kanuni hiyo kule
Mtwara, mambo yaliwatokea puani ,mwaka huu.Cha ajabu sana,mtu mmoja
akitokezea,kiushauri au kuipinga serikali,akiwa na mawazo
endelevu,shukrani yake ni kuambulia risasi ya moto,na tetesi za kifo
chake zitatolewa kwamba , KAUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.Mi nahisi Tanzania
inaweza kuonja vita ya ndani miaka ijayo......
Hatuhitaji nidhamu ya woga au chuki dhidi ya ukweli kuweka wazi mambo haya, kwa kuwa tayari yapo katika serikali yetu. Tuzidi kupigana kwa falsafa ya namna hii kwa kuwa bado tunadhaniwa kama watu wa chini, ila ipo siku, our ACTIONS WILL SPEAK LOUDER THAN WORDS!
ReplyDelete