Rais wa Venezuela Hugo Chaves hatimaye amefariki usiku wa kuamkia leo baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa muda sasa, Hayati Hugo Chavez alipata matatizo ya kansa mara baada tu ya uchaguzi wa nchi hiyo hali iliyomfanya ashindwe hata kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake. Alienda kupata matibabu katika nchi ya Cuba na baadaye mapema mwezi huu kurudishwa nchini mwake. Chavez amefariki akiwa na umri wa miaka 58 na alikuwa kiongozi wa Venezuela tangu mwaka 1999. Kifo cha rais huyo aliyekuwa kipenzi sana cha watu wake kimeleta simanzi kubwa miongoni mwa raia wa nchi hiyo japokuwa walitarajia kusikia habari za kifo chake baada ya raisi huyo kuugua kwa muda mrefu. Raia wameonekana wakiwa katika mitaa ya mji wa Carcas wakimlilia kiongozi wao. Taarifa za kifo cha kiongozi huyo zimetangazwa na makamu wa rais wa nchi hiyo. Bongonewz tutaendelea kuwapa updates za yale yanayoendelea katika msiba huo..
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII