HATIMAYE DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU KUMUOA PENNY......SOMA PIA ALICHOMFANYIA HIVI SASA
Soudy Brown alimuuliza kuhusu fununu za kutumia Milioni 15 kununua gari la mke wake mtarajiwa mtangazaji Penny ambae kwa sasa ni mjamzito.
Diamond amekiri kwamba ni kweli kamnunulia Penny gari kwa sababu anaelekea kuwa mama watoto ambapo namkariri akisema “nilimuuliza gari gani anapenda, nimemuagizia iko njiani inakuja kwa hiyo sasa hivi anatumia la muda wakati akisubiria gari lake”
Alipoulizwa kuhusu kumuoa na kama mtoto atazaliwa nje ya ndoa, Diamond amejibu “siwezi kusema lini ila Mwenyenzi Mungu ndio anajua inaweza ikawa harusi ila kuna time inafika inabidi utulie, siwezi kusema chochote kwa sababu inawezekana mtoto akazaliwa ndani ya ndoa pia “
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII