Pages

Monday, March 18, 2013

KATIKA PICHA : HIVI NDIVYO TRAFFIC ALIYEKUWA AKIONGOZA MSAFARA ALIVYOGONGWA HADI KUFA....TAZMA PICHA NA USOME PIA


Trafiki wa kike aliyejulikana kwa jina moja la Elikiza aliyekuwa akiongoza magari eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar, akifunikwa na wasamaria wema baada ya kugongwa na gari na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo.
Trafiki Elikiza baada ya kugongwa na gari eneo la Bamaga muda huu.
Baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio.


Hali ilivyokuwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.

Trafiki mmoja ambaye amefahamika kwa jina moja la Elikiza, muda huu amegongwa na gari aina ya VX ambayo haikujulikana namba na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo wakati akiongoza magari eneo la mataa ya Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam. Taarifa zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa Trafiki huyo alikuwa akiongoza msafara na baada ya msafara huo, aliruhusu magari mengine yaendelee na safari ndipo ghafla gari lilipotoka upande wa pili na kumgonga.  
 
Shuhuda aliyekuwapo katika tukio hilo ajulikanaye kwa jina la WillyIam anasimulia : Ndugu zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha na yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance.


Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:
Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so akawasimamisha mungu saidia alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. Bila ya kuangalia nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from Shekilango road na hapo ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na speed kama 120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna magari yanayo-cross from Shekilango.

Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC badala ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala hamadi traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona sekunde ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila baada ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia sasa na wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua si kitu kizuri kutazama.

Ila nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule mama nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta.

Binafsi nimechukulia kama fundisho kwangu, sina mtazamo kama wa wachangiaji wengi wa juu yangu.

(Picha na Shauri Kati / GPL)

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII