UCHAGUZI WA PAPA: MAKUNDI YAIBUKA MIONGONI MWA MAKARDINALI....SOMA ZAID HAPA
Vatican City.
Dirisha limefunguliwa tayari kwa hewa safi kuingia Vatican City. Hivi ndivyo unavyoweza kuuelezea mchakato wa kumpata Papa wa 226 wa Kanisa Katoliki, unaoanza leo.
Mchakato huo unaanza rasmi saa 10.45 jioni kwa saa
za Vatican (Saa 12.45 kwa saa za Afrika Mashariki) na utatanguliwa na
ibada maalumu ya misa ya makadinali 115 wanaoshiriki katika uchaguzi
huo.
Tayari, vumbi limeanza kutimka huku makundi
makubwa matatu yakiibuka katika uchaguzi huo, unaofuatiliwa kwa karibu
kote duniani na ambao unaweza kudumu hadi wiki mbili.
Makundi hayo ni pamoja na lile la makadinali wa
Italia, wapatao 28 dhidi ya Wamarekani 11, wote wakiwa na malengo
tofauti katika nia yao ya kuchukua wadhifa huo wa juu katika Kanisa
Katoliki.
Hata hivyo, Italia ina mgawanyiko mkubwa wa
vikundi vya kiitikadi miongoni mwa waumini wake, kama ilivyo kwa
makadinali hao, jambo ambalo linapunguza umoja wao.
Wataliano kwa upande mwingine, wangependa kumaliza
miaka 35 ya utawala wa wageni katika Vatican tangu alipoingia Papa
Yohane Paul II mwaka 1978 (sasa mwenyeheri) na mfuasi wake, Benedict XVI
na hivyo kurejesha miaka zaidi ya 450 ya utawala wao katika kiti hicho
cha Mtakatifu Petro, wakipenda pia kudumisha mazoea ya utawala wa
kirasimu katika uongozi huo.
Tofauti na miaka ya nyuma, wachambuzi wa masuala
ya dini na imani, wanaona kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mwepesi zaidi
kwani hakuna kadinali mwenye nyota zaidi ya wengine miongoni mwa
washiriki hao 115, ambao angepewa nafasi kubwa kuibuka mshindi.
Hata hivyo, Wamarekani, taifa kubwa na tajiri
duniani wanaowakilishwa na makadinali 11, imani yao ni kutaka kuupeleka
nchini mwao, uongozi wa Vatican. Dhamira yao, pia inapingwa.
Hao wanadhani kuwa Marekani haiwezi kutoa kiongozi
mkuu wa kanisa hilo, ambaye ataweza kukabiliana na wapinzani wa Ukristo
na kuaminika kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Kundi lingine na ambalo linaweza kubadili matokeo, ni la wateule 67 wa Papa Benedict ambao ni zaidi ya nusu ya wapigakura wote.
Wao wanaelezwa kuwa mchango wao katika uchaguzi
huo utakuwa mkubwa na hata kuathiri matokeo, kama watapenda kuendeleza
misingi ya uongozi wake.
Pamoja na makundi hayo, kuna baadhi ya makadinali ambao kura ya maoni, imeendelea kuwabeba zaidi kabla ya uchaguzi wenyewe kuanzia leo.Watu wa kundi hilo wanaongozwa na raia wa Brazil, Odilo Scherer, ambaye anasemekana kuwa karibu na mfumo wa kanisa hilo, Curia, anapigiwa upatu na Wataliano.
Source : MCL
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII