Pages

Saturday, April 6, 2013

HUYU NDIYE BIBI WA MIAKA 76 ANAYEDAI KUWA AMEPEWA UJUMBE NA MUNGU AMFIKISHIE RAIS KIKWETE...!!

Amani usiamini! Bibi kizee Veronica Amos Kayombo (76), mwenyeji wa Ludewa, Njombe anayeishi Buza, Dar, amedai kuisikia sauti ya Mungu ikimuagiza akaonane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ampe ujumbe muhimu, shuka nayo.

MAHOJIANO MAALUM
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum mwanzoni mwa wiki hii akiwa nyumbani kwake Buza, Bibi Veronica alisema amekuwa akitokewa na Mungu mara kwa mara na kumpa maelekezo mengi ambayo anatakiwa kuyatoa pale atakapofika kwa Mheshimiwa Rais Kikwete.

 
ATOKEWA NA TASWIRA YA MUNGU
“Nimekuwa nikitokewa na taswira na sauti ya Mungu, kwa idadi inaweza kufika mara saba na kuambiwa
kuwa nisiondoke Dar, bila kuonana na Kikwete ili nimpe zawadi zake ambazo nimezitunza kwa muda mrefu na siri iliyoko moyoni ambayo nimepewa na Mungu,” alisema bibi kizee huyo.

 
KWA NINI JK?
Aliendelea kusimulia kwa masikitiko kuwa zawadi atazompatia JK ni kwa ajili ya kumpongeza kwa kuweza kuwasaidia albino, watu wasiojiweza, wazee na kutuliza vita nchini Kenya na Uganda ambazo zilikuwa zimejifichwa kwani nchi nyingine kama Rwanda na Burundi zilikuwa wazi.




ANATOKEA NJOMBE
Bibi Veronica alifika Dar akitokea Njombe kwa ajili ya mazishi ya mama yake mdogo na baada ya kumaliza msiba alijiandaa kuondoka lakini Mungu alimtokea 6:00 mchana na kumweleza kuwa asiondoke hadi atakapoonana na JK.

 
ATUMIA MKWANJA MREFU
Baada ya hapo amekuwa akifanya jitihada za aina mbalimbali kwa ajili ya kuonana na rais lakini hadi sasa hajafanikiwa kwani ameshapoteza fedha nyingi kwa kuwahonga watu ili wamfikishe Ikulu pale Magogoni, Dar na kutoa kopi za barua kwa ajili ya kuomba maombi ya kukutana naye.
“Nimepoteza fedha nyingi sana kila ninayekutana naye ananiambia atanipeleka lakini nimpatie fedha, natoa mpaka sasa nimeishiwa, nimeshaenda mpaka ofisi zote zinazohusika na kuwakutanisha watu na rais lakini sikufanikiwa, watu wamekuwa wakiniona chizi lakini nina akili zangu timamu na maono haya ni ya Mungu kwani mbali na kuambiwa pia la kufanya nikifika huko lipo kwenye kitabu hiki (anaonesha Biblia).
Bibi kizee huyo alipoona ameshahangaika huku akizuia kila mara kuingia Ikulu, aliamua kuita vyombo mbalimbali vya habari na kufikisha ujumbe wake ambapo mbali na hapa gazetini pia radio zitarusha matangazo yake moja kwa moja yatamfikia Rais Kikwete.

 
AMPA ZAWADI LOWASSA, MKAPA
Kwa mujibu wa bibi Vero, aliwahi kukutana na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye alimpatia gunia la mahindi na zawadi za Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na mkewe Mama Ana Mkapa alipokuwa kwao Njombe.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa mama huyo wakati anatoa zawadi hizo alioneshwa kwenye vyombo vya habari ambapo alitoa kitenge cha mama, gunia la mahindi na zawadi ya rais

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII