Pages

Tuesday, April 23, 2013

MR NICE AFUNGUKA NA KUDAI ANABEEF NA WATANZANIA.....AELEZEA NIA YAKE YA KUOA KENYA...SOMA STORY KAMILI HAPA

Msanii mkongwe aliyekuwa amepotea kwenye chart nchini, Nice Lucas Mkenda ameendelea kutengeneza vichwa vya habari nchini Kenya baada ya jana kuhojiwa kwenye vituo vikubwa vya runinga nchini humo, Citizen TV na NTV.

Katika kituo cha Citizen, Mr Nice ambaye amesainishwa kwenye label ya Grandpa Records, alikuwa akihojiwa live kwenye muda wa taarifa ya habari ya jioni kwa lugha ya Kiswahili inayotazamwa na watu wengi nchini humo na hata Tanzania huku kwenye NTV akionekana kwenye kipindi cha comedy cha The Churchill Show. Haya ni miongoni mwa yale aliyoyaongea Citizen TV.

Kuhusu sababu za kwenda Kenya
Nilikuwa nimesimama muziki muda mrefu kama miaka minne hivi na baadaye nikakutana na kampuni ya GrandPa Records. 


Kwakweli walinifuata Dar es Salaam tukaongea maneno mengi ya busara sana kwasababu wao naona wanaona mbele zaidi. Wakaniambia Mzee ‘we umekaa kimya muda huenda ni sababu ya hasira lakini bado watu wanakuhitaji sana kwahiyo kuna vitu vingine hata kama vilikukwazwa vinaweza vikatatulika kwasababu unangojewa tu haujawa wa zamani, bado wewe ni mpya’. 


Nimekaa nyumbani 4 years lakini kaja mkenya, kanifuata kwa gharama nyingi sana na kunishawishi you must come back again! kwahiyo nasema wakenya asanteni sana kwa yote mliyonifanyia .

Kuhusu kama ana beef na watanzania

Hapana mimi sina beef na watanzania wenzangu kwasababu kwanza kazi ya muziki ni yangu sio ya watanzania na kila mtanzania ana kazi yake, kila mkenya ana kazi yake. 


Kwasababu hata kuna wakenya wanafanya kazi Tanzania wapo Tanzania na walifuatwa hapa Kenya kwenda kufanya kazi Tanzania. Nimekumbana na maswali mengi kwenye interview ‘kwanini usifanye na kampuni za Tanzania? 


Nikasema walioniona na wakaona kwamba nahitajika, ni mkenya ndio alikuja kunifuata so ningeacha kufanya naye kazi? Na akanipa faida zake.

Kuhusu wimbo wa Mack Muga wa Ali Kiba

Ali kiba ni mdogo wangu, rafiki yangu na hatujawahi kukorofishana hatujawahi kuwa na beef ya aina yoyote hata sijawahi kumsikia akinizingumzia mahali kwa ubaya. 
 
Haya ninayoyasema hapa , hizo ni story kichaa kwasababu nimeizunguka sana dunia kwakweli, passport yangu inatisha, unaifungua kama gazeti lakini bahati nzuri ama mbaya mimi sijawahi kufika South Africa hata siku moja na wala sijawahi kufanya hata interview na kituo chochote.  
 
Na hiyo nimeisikia hapa Kenya hata Tanzania sijawahi kusikia kitu kama hicho.
 
Kuhusu kuoa
Nadhani ni moja kati ya mambo yaliyonileta hapa nimekuja pia kuoa Kenya, short and clear , atapatikana na nitawaambia hayo ni mambo ya kumwachia Mungu.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII