Pages

Friday, April 12, 2013

SOMA RIPOTI YA TUME ILIYOAUNDWA KUCHUNGUZA KUFELI KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2010 AMBAYO ILIWEKWA KAPUNI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA 4 MWAKA 2010
Dar Es Salaam
Juni, 2011

SHUKRANI
Utafiti huu umehusisha wataalamu mbalimbali katika hatua za kubuni, kutayarisha, kukusanya, kuchambua takwimu na kuandika ripoti. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa pamoja zinawashukuru wataalamu wote waliohusika kwa njia moja ama nyingine katika hatua mbalimbali za utafiti huu. Pia tunawashukuru wadau wote wa elimu waliohusika katika kutoa taarifa za utafiti. Aidha shukrani za pekee ziiendee Wizara ya Fedha kwa kufanikisha mchakato mzima wa utafiti. Shukrani pia zimwendee Bwana Jumanne Abdallah Sagini, Naibu Katibu Mkuu - TAMISEMI kwa kuwa msimamizi mkuu wa kazi hii. Aidha, shukrani za dhati ziwaendee
wajumbe wa kikundi kazi kilichohusika katika utafiti huu kuanzia hatua za awali hadi mwisho. Wajumbe hao ni:
JINA TAASISI WADHIFA
1. Francis M. Liboy OWM-TAMISEMI - Mwenyekiti
2. Lawrence John Sanga WEMU - Katibu
3. Fred Davidson Sichizya WEMU - Mjumbe
4. Abdallah Shaban Ngodu WEMU - Mjumbe
5. Hadija Mchatta Maggid WEMU - Mjumbe
6. Paulina Jackson Mkoma WEMU - Mjumbe
7. Elia Kalonzo Kibga WEMU - Mjumbe
8. Paulina Mbena Nkwama OWM-TAMISEMI - Mjumbe
9. Makoye J.N. Wangeleja TET - Mjumbe
10.Edward Simon Haule NECTA - Mjumbe
Aidha shukrani zimwendee Mkurugenzi Mkuu wa TET kwa kugharamia vikao vya kikundi
kazi kupitia huduma ya ukumbi na chakula wakati kikiwa Dar-es-salaam.
Prof. Hamisi O. Dihenga
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
DIBAJI
Ripoti hii ya utafiti inahusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 mwaka 2010. Utafiti huu umefanywa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU) ikihusisha Taasisi ya Elimu Tanzania na Baraza la Mitihani la Tanzania. Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri kwa wadau wa elimu Serikali iliamua kufanya utafiti ili kuweza kubaini chanzo na ukubwa wa tatizo. Utafiti huu unatoa mapendekezo kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu na ubora wa elimu ya sekondari.
Ripoti hii inaonesha kwamba yapo masuala ya kimfumo, mfano mapungufu katika usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini ambayo yanaweza kutatuliwa na serikali moja kwa moja. Aidha, yapo masuala yanayohusu kujenga uwezo kwa wasimamizi na watekelezaji wa mitaala, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa bora na vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia na uboreshaji wa majengo na miundombinu ambayo yanahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wabia wake.
Matokeo ya utafiti huu ni muhimu kwa serikali, washirika wa maendeleo na wadau mbalimbali wa elimu kwani inaonesha chanzo na ukubwa wa matatizo na changamoto zinazojitokeza na inatoa mapendekezo ya namna ya kuyatatua na kukabiliana na changamoto za kielimu. Hivyo sote kwa pamoja yatupasa tujipange na kuelekeza nguvu zetu kupitia mipango yetu ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili tuweze
kuyamaliza matatizo haya na kuinua ubora wa elimu nchini. Ninawaomba wadau wa elimu nchini kuyafanyia kazi matokeo ya utafiti huu ili kuweza kupiga hatua katika utekelezaji wa utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi. Serikali inayo nia ya dhati ya kutekeleza mapendekezo haya ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu ya sekondari nchini.
Mh. Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (MB)
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

KUSOMA RIPOTI KAMILI BOFYA HAPA NA UNAWEZA KUIDOWNLOAD PIA

                                                  BOFYA HAPA KUSOMA RIPOTI NZIMA

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII