UNAJUA ALICHOKISEMA MAMA KANUMBA KUHUSU LULU??? SOMA HAPA
Mama
wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amesema anampenda msanii Elizabeth
Michael maarufu kwa jina la Lulu, licha ya matatizo yote yaliyotokea na
kwamba anamwachia Mungu katika yote.
Akizungumza na Mwananchi katika makaburi ya
Kinondoni mara baada ya misa maalum ya kumuombea marehemu na kuweka
mashada ya maua Mtegoa alisema yeye ni mkristo hivyo hana kinyongo na
mwigizaji huyo.
"Mimi ni mkristo tumeambiwa samehe mara saba
sabini, binafsi sina kinyongo chochote na ninampenda kama ilivyokuwa kwa
mwanangu, ila kila ninapomuona siachi kumkumbuka mwanangu," alisema
Mtegoa.
Alisema Kanumba alikuwa ni kama mtoto, mume, kaka
na kama rafiki yake, alimfanya kuwa mtu wa karibu yake na anashukuru
mwanaye pia alimfanya ajisikie furaha muda wote.
"Mara ya mwisho kuongea naye ilikuwa ni Aprili 6
usiku, siku moja kabla ya kifo chake, tulizungumza mengi kwa njia ya
simu aliniahidi mengi na kunieleza kuhusu safari yake ya Marekani,
nammisi kwa kweli," alisema.
Akizungumzia suala ya ushiriki wake katika filamu
ya Without Daddy Mtegoa alisema "Nilikuwa naigiza tangu nasoma
sekondari lakini sanaa hapo nyuma haikulipa hivyo sikuendelea na sanaa,
baada ya kufariki Kanumba niliombwa nicheze filamu ya Without Daddy,
nilikubali na ikawa filamu yangu ya kwanza," alisema.
Alisema kwa sasa yeye anafanya kazi chini ya
Kampuni ya Kanumba The Great, hivyo itakapotokea filamu nyingine yupo
tayari kuicheza.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII