HII NDO LIST YA WATU MAARUFU KUTOKA KENYA NA TANZANIA, AMBAO WAMETAJWA NA MTANDAO WA KENYA KUA NI MAFREEMASON. WOLPER NAE KATAJWA
Inawezekana kila kitu kina wakati wake, kuna muda watu
walikuwa wakisikia neno ‘Freemason’ ama ‘Illuminate’ kama inavyojulikana nchini
Kenya wengi walikuwa wanaiona ni habari kubwa, lakini kwa sasa hivi inaweza
kuchukuliwa kama sio big deal.
Sababu ni ile ile kuwa wengi wanaoendelea kwa haraka ama
kuwa juu katika kile wanachokifanya basi utasikia huyo ni member wa Freemason,
kwa upande wa Marekani wanasema ‘he/she just sold her/his soul to the
devil’. Japo kwa upande wa Marekani wapo
wanaokiri kufanya hivyo kweli, ila kwa Africa Mashariki hakuna msanii aliyewahi
kukiri.
Lakini yote hayo ni kama yanakanganya na kuonekana kama
hayana mantiki hasa pale ambapo vithibitisho vya kinachoongelewa huwa havileti
mantiki ya moja kwa moja. Pengine watu wanatafuta pesa kwa bidii na kumuomba
Mungu lakini kwa kuwa kwenye mstari wa juu wanajikuta wanahisiwa kuwa member wa
secret society (Freemason). Oh..au labda ndo vile kwa upande mwingine lisemalo
lipo na kama halipo laja !
Tunathubutu kuziita blaa blaa kwa upande mwingine, lakini
tukiweka kwenye mabano kuwa inaweza kuwa na ukweli, who knows!
Mtandao wa malimwengu wa nchini Kenya huenda ukawa na mfano
mzuri wa kile nilichokitaja hapo juu, mtandao huo kupitia mwandishi wake
imetaja majina ya wasanii wa Tanzania na Kenya wanaosemekana kuwa ni wafuasi wa
Freemason, lakini kizuri zaidi ni kwamba mtandao huo umejaribu kuonesha
vithibitisho na kushindwa kupata jibu la moja kwa moja kwa nini wasanii hawa
wamekumbwa na hili. Inabaki hivyo hivyo kuwa tetesi tu.
Hawa ni wasanii waliotajwa na maelezo yanayowahusu:
TANZANIA:
1.Naseeb Abdul
Jumaa (Diamond Platinum)
Picha aliyopiga mwaka jana akiwa na mzungu anaeaminika kuwa
ni moja kati ya viongozi wa Freemason wakiwa wameweka pozi na kuonesha ishara
inayooaminika kuwa ni ya Freemason, na kwamba alipoulizwa yeye alisema
hakufahamu kama alikuwa anaelekezwa kupiga picha kwa pozi la ki-freemason. Kwa
mujibu wa mwandishi anaona inaweza kuwa kweli kwa sababu anaonekana kuenjoy!
2.Ali Kiba
Iliwahi kusemekana pia kuwa Ali Kiba ni Freemason, na wewe
pia unaweza kufikiria sababu kwamba eti alikuwa maarufu sana na baadae kufifia.
Maoni ya mwandishi (Hakuna uthibithibisho/ushaidi unaoweza kuwekwa thidi yake).
3.Jacquelin
Wolper
Ni muigizaji maarufu wa kike mtanzania. Maoni ya mwandishi (
Hakuna ushaidi, tetesi peke yake hazina umuhimu)
KENYA:
1.Camp Mulla
Maoni ya mwandishi (Hapana, sio kweli. Sababu ya kufanikiwa
kwenye muziki haimaanishi kuwa ni members wa Freemason. Hakuna mtu mwenye
ushahidi kuwa Camp Mulla ni members wa Freemason).
2.Octopizzo
Maelezo yanayomhusu yanaonekana kuwa mengi sana kama
kawaida, ni moja kati ya wasanii ambao tetesi za kuwa illuminate ni nyingi
zaidi.
3.Nonini
Ukimtaja Nonini kama Illuminati lazima kitu serious zaidi
kiandikwe ama ikielezwe. Nonini sio Illuminati (maoni ya mwandishi).
Hao ndio waliandikwa na kutolewa maoni ama maelezo na
muandishi wa mtandao huo. Lakini tetesi huwa nyingi na kuongezeka mara kwa mara
kwani hata Avril pia huwa anatajwa kuwa Illuminati na kwamba kazi yake ni
kueneza usagaji nchini humo na eti sababu mojawapo ni mashairi ya wimbo wake
‘Chokoza’.
Haya yote yanasemwa tu, cha kufanya ni kile alichokisema
Prof. Jay kwenye wimbo wake ‘Bongo Dar es Salaam’... “Akili kumkichwa, ukizubaa unaachwa feli”.
Nami nakiri na kurudia huo usemi usemao LISEMWALO LIPO KAMA HALIPO BASI LINAKUJA
ReplyDelete