Pages

Thursday, May 16, 2013

HUYU NDIO MWALIMU WA CHUO KIKUU AMBAYE PIA NI MSANII WA BONGO FLEVA....SOMA NA USIKILIZE NGOMA ZAKE PAMOJA NA INTERVIEW


Majina yangu halisi Issaya Lupogo, jina la kisanii Lupogezzle.
Kazi yangu ni mwalimu wa chuo kikuu cha Mzumbe-Tanzania, ila kwa sasa niko masomoni ambapo nafanya digrii ya udhamiri ya Lugha (M.A.Linguistics) katika chuo kikuu cha Dar essalaam.
Muda wangu wa ziada nafanya sanaa,muziki wa bongo flavour. Nyimbo zangu ambazo ziko hewani kwa sasa ni "Ufisadi" na "Issaya & Aziza".

Mtazamo wangu wa Muziki hususani muziki wa kizazi kipya:
kufanya muziki huo sio uhuni, uhuni ni tabia ya mtu ambayo hufanywa sio na wasaniii tu bali hata watu ambao tunawaheshimu na kuwaamini katika jamii yetu. Mfano ni mara ngapi tunasikia waheshimiwa wakubwa wamenaswa na vimada? ni mara ngapi tunashuhudia walimu wakiwapa mimba wanafunzi mashuleni.
Malengo yangu katika muziki wa kizazi kipya (bongo flavour): Kuunganisha wasanii wote wa Tanzania na kupanga ili tuweze kuwa na chanma chetu cha wasanii kitakachotambulika ambacho kitatetea haki zetu (Wasanii). Nimejaribu kuunda kundi ktk Facebook liitwalo "UWABO" Umoja wa Wasanii Bongo, lakini bado halijapata wadau wengi, kama tujuavyo wabongo kila mtu anataka kufanya mambo peke yake.

Ushauri wangu kwa wasanii wenzangu: Wajiamini wsifanye kazi kwa kuogopa. Pia tusijikite kuimba Mapenzi tu, tuimbe masuala yote yanayolihusu Taifa Letu. Nawapongeza sana wasanii kama Mrisho Mpoto, Roma na Afande Selle ambao wamekua wakigusa na sehemu zingine tofauti na mapenzi.

Mwisho: DAWA YA KUTOKOMEZA UNYONYWAJI NA UONEVU WA WASANII NI KUUNGANA KWA KWA WASANII WENYEWE NA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA HUKU WAKISHIRIKIANA, WAKIJIHESHIMU, KUSHAURIANA, KUSAIDIANA NA KUPENDANA.

HIZI NDIO BAADHI YA NYIMBO AMBAZO LUPOJIZO AMEFYATUA MPAKA SASA....UNAWEZA KUDOWNLOAD NA KUZISIKILIZA HAPA PIA

UFISADI BY LUPOGIZLE


INTERVIEW YA LUPOGIZLE AKIHOJIWA JUU YA MUZIKI NA MAISHA YAKE KIUJUMLA

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII