KUA WA KWANZA KUSIKILIZA NA KUDOWNLOAD WIMBO MPYA WA TMK HALISI, HUU NDO ULE WIMBO AMBAO NATURE KAMCHANA SAM MISAGO
Leo hii Nature akiwa na kundi zima la TMK Halisi (Dolo, Kr, Jb wa
mabaga na yeye mwenyewe), wameachia wimbo mpya unaoitwa "Fitina" ambapo
ndani kuna mistari kwenye verse ya Nature inayoonyesha kumchana mmoja
wa watangazaji wa Kituo cha Televisheni, kilichositisha mahojiano nae
baada ya kuingia studio akiwa na ndala na kawosh
"halafu watu wengine wanakuwaga sijui ni mapimbi, eti msanii kaingia studio na ndara
na amevaa pensi, hakujua anayoyasema, kwenye facebook na twitter
sijui kisa hela alizopewa, na mameneja feki, wasiopenda wauswazi, mzomeeni huyoooo
oooooohhh"
Nature pia amezungumzia ujio wa ndala za halisi wiki ijayo akiwa na kampuni ambayo hajaitaja jina
"ebana eeeh mi nnachosema watu wngu wote wajiandae kabisa, maduka
watayapata sehem zote na katika vile vituo maalum kabisa vya watu
kujaa,na ndala zitakuwepo na tutawatagazaia zaidi kwasababu wiki ijayo
nadhani ndio zitatoka kwasababu bado tunafanya contract, staki kuongela
zaidi sasa hivi lakini naimani watu watapenda..
sema kitu kimoja mavazi ya mtanzania ukizingatiaaa, aah usimjaji mtu eti
kisa kwasababu amevaa kitu flani, niangali mimi ni msanii wa zamani,
kwahiyo mimi sitaki kuji shshow show, mi nafanya kazi ukweli , kama
nikijua leo naenda kwenye Fiesta nalipuka, kama nikijua naenda kwenye
tamasha kubwa nalipuka kama niitwa na muheshimiwa Jakaya Kikwete, lazima
nilipuke umenieelewa bwana.
lakini sasa mimi nimeenda kama mkubwa, na ukiangalia katika ile nyimbo
ambao nimefanya mimi, ni mimi mtoto wa uswahilini na Tundaman,Tundaman
ndio inatakiwa sasa hivi alipuke, si tunaenda kifaza, sie wakubwa,
utafauti uonekane, hasa we unafikiri anavyovaa Nature na mzee ngurumo ni
sawa "
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII