RAMA MLA WATU AACHIWA HURU....SOMA HABARI KAMILI


Ramadhan Suleiman ‘Rama mla watu’ akiwa mahakamani leo.
Mama mzazi wa Rama mla watu, Khadija Ally, akiwa mahakamani kabla ya kuachiwa huru.
Rama akitafakari jambo ndani ya mahakama.
Mawakili wakijadiliana jambo baada ya kesi hiyo.
Rama katika pozi mahakamani.
KIJANA Ramadhan Suleiman Mussa ‘Rama mla watu’ na mama yake Khadija Ally, leo wameachiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  baada ya kubainika kuwa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo (mla watu) alifanya kosa la mauaji akiwa na matitizo ya akili. Hata hivyo Rama Mla Watu, ataendelea kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Isanga mkoani Dodoma mpaka akili yake itakapokuwa sawa ndipo ataachiwa kuwa huru mtaani ili asije akawadhuru watu wengine. Khadija Ally yeye ameachiwa huru. Rama alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa ni cha mtoto Salome.
(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)
Zifuatazo ni baadhi ya taswira za Rama mla watu enzi hizo:
Rama na mama yake, Khadija Ally wakipelekwa mahakamani chini ya ulinzi mkali baada ya kukamatwa kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Salome yaliyotokea Aprili 25, mwaka 2008.
Rama akihojiwa.
Mama mzazi wa mtoto Salome Yohana (3) akilia kwa uchungu wakati wa mazishi ya mwanaye.
Rama na mama yake wakiwa mahakamani.
Rama akiwa kalala kwenye majani.

CREDITS : GPL
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs