-Barabara zimewekwa vizuizi, magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita.
-Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake. Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
- Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao. Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
-Mahakama ya mwanzo ya Mitengo nayo imechomwa moto.
-Mwanafunzi wa CHUNO afikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
-Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari Magereza na uhalifu ukifanyika vidole vinawaelekea Polisi.
-Mabomu yanaendelea kupigwa tofauti kwa sasa hayapigwi mfululizo.
-Mabasi matano ya Champion yaliyobeba wanajeshi yako njiani yanaelekea Mtwara.
-Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
-Bunge laahirishwa tena kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
-RPC aongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende kazini. Lakini kiuhalisia hali bado sio shwari
Chanzo: MTWARA KUMEKUCHA BLOG
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII