Pages

Monday, June 24, 2013

Mhadhiri wa chuo kikuu amtetea Ommy Dimpoz na kusema kilichomponza ni kutojua kujibu maswali ya waandishi wa habari.




Huyu ni mhadhiri wa chuo kikuu cha mzumbe na pia ndio yule mwl wa chuo kikuu anayefanya bongo fleva.


Yeye kama Msomi mzuri na mwalimu wa wasomi wa chuo kikuu,ameona kabisa Ommy Dimpoz hana makosa kabisa na amewaomba watanzania wamuelewe Ommy Dimpoz na kumsamehe.

Haya ndio maneno ya huyu mhadhiri wa chuo kikuu Issaya Lupogo jina la kisanii Lupojizo.

''Binafsi nasikitishwa sana na mashabiki kumfanyia Ommy Dimpoz mambo haya mabaya. Nilimsikiliza sana Ommy Dimpoz siku ya KTMA, hakumaanisha kama watu suku hizi wanavyotafsiri.
Alichikisema Ommy kwa namna nyingine kinaweza kutafsiriwa kama wadau na serikali zitoe kipaumbele na kuthamini kazi za wasanii wa nyumbani ili wasanii wanufaike zaidi na siku ya mwisho wasife masikini. Huu ni ukweli kabisa kuhusu hali iliyopo kwa wasanii sasa. Wasanii wananyonywa na kudhulumiwa, mwisho wa siku msanii anaishia kupata umaarufu tu usio na kitu chochote.
Kingine nilichokiona ni Ommy D kutotetea hoja yake pindi alivyohojiwa na waandishi wa habari, badala ya kueleza hoja hiyo kiumakini alijikuta aikbabaika na kukumbilia kuomba msamaha.

Jambo alilolisema Ommy D lilisemwa pia na Afande Selle na Mr. Sugu siku ya kuaga mwili wa Ngwair uwanja wa Jamhuri morogoro, kama ni hvo basi mbona hao hawakuandamwa kama Ommy D?

Watanzania tuwe waelewa,wasanii wengi wa Tanzania bado ni masikini, kipatao wanachokipata hakiendani na kazi wanayoifanya na umaarufu walionao, hii sio kwa Ngwear tu bali kwa wasanii wengi wa Bongo. Sababu ni unyonyaji na udhulumaji uliopo wa kazi za wasanii, na serikali kutoweka mkazo juu ya kuangalia maslahi ya wasanii nchini.
Nawaomba watanzania tusiendelee kumsakama Ommy D, na Ommy D naomba uwe unajaribu kujenga hoja vizuri kwa kile unachokisema na sio kukimbilia kuomba msamaha bila hata ya kutenda kosa lolote.''

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII