KUTOKA JAMII FORUMS : DR. MAGUFULI v/s ZITTO KABWE SAKATA LA TSHS. BIL 252

 
Napata shida na hoja ya Mh.Zitto kuhusu upotevu wa hela anaodai wizara ya Ujenzi wamekula, anahoji fungu zima bila kuainisha ni miradi ipi(aitaje kwa majina) iliombewa fedha hizo special na kupitishwa na bunge. Nasema hivyo itakuwa sasa ni vyema wizara ikaulizwa kama miradi hiyo haikuwekewa fedha hizo kama ilivyoidhinishwa, mfano fedha zilitengwa ili kuanza ujenzi wa miradi mipya(ataje mradi mjo baada ya mwingine)mpaka mwisho na tujumlishe tupate hizotsh 252 bilioni. Nahisi hili ni gumu kwa Zito ila atakimbilia kusema tulipitisha fungu zima bila kuainisha miradi (mradi mmoja mmoja). Ndo maana wizra ya ujenzi wameweza kudhibitisha na kufafanua madeni walivyolipa kwa klla mradi na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali keshasema hayo nitanukuu sakata lilivyoanza bungeni, Dr.Mgufuli akijibu hoja ya Zitto, barua ya katibu mkuu wizara ya ujenzi kwenda kwa vyombo vya habari na pia nitawanukuu wabunge wa upinzani wakimsifu Dr.Magufuli na kuacha ili tujadili ili kujua ni nani tumwamini katika hili, haya kazi twende:

1. HOJA YA ZITTO KABWE NA MAJIBU YA DR.MAGUFULI
https://www.youtube.com/watch?v=WeY97J07RoQ



2. MAJIBU YA WIZARA YA UJENZI:

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Yah: USAHIHI WA MATUMIZI YA KASMA MAALUM YAUJENZI WA MIRADI YA BARABARA NCHINI SHS. 252,975,000,000.00


Tarehe 22/08/2013, Wizara ya Ujenzi ilikutana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa ajili ya kujadili Hesabu zilizokaguliwa za Fungu 98 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012. Kikao hicho kilifanyikia katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Mhe. Gaudence Cassian Kayombo Mbunge wa Mbinga Mashariki, ambaye alitoa maamuzi na maelekezo rasmi ya Kamati.

Katika kikao hicho hoja kadhaa zilijadiliwa ikiwamo hoja kuhusu Matumizi ya Kasma Maalun ya Ujenzi wa Miradi ya Barabara nchini ambayo ilitengewa kiasi cha Shs. 252,975,000,000.00.

Katibu Mkuu (Afisa Masuhuli) wa Wizara ya Ujenzi alikiarifu kikao hicho kuwa fedha za Mradi huo Maalum zilitumika kwa ajili ya kulipia madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri kwa miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea katika mipango na bajeti ya Serikali. Katika ujenzi wa barabara; jukumu la msingi kwa Wizara ni kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri.

Aidha, alifafanua kwamba Mradi huu umekuwa na matokeo mazuri kwani ulifanikisha shughuli za ujenzi wa barabara nchini. Afisa masuhuli aliendelea kufafanua kwamba mradi huu wa barabara haukuwa mradi kivuli bali ulikuwa ni mradi maalum kwa lengo la kufanikisha programu ya barabara na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.

Tarehe 22/08/2013 na tarehe 23/08/2013 zimetolewa taarifa za upotoshaji na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu ukweli wa suala hili ambapo baadhi ya vyombo hivyo vilinukuliwa kusema kuwa kumekuwepo na ufisadi, matumizi tata na ubadhirifu katika mradi huu.

Wizara inapenda kuudhibitishia umma kwamba katika utekelezaji wa mradi huu hapakuwepo na ufisadi, ubadhilifu, au matumizi tata.

Ukweli huu umethibitishwa kwa maandishi na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwamba hoja ya ukaguzi huu haikuhusu ubadhirifu au matumizi mabaya yoyote ya fedha bali ni suala la uandishi wa vitabu vya fedha uliohitaji kuboreshwa.

Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa ufafanuzi huu na kuudhibitishia tena umma kwamba hakuna upotevu wowote wa fedha kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimetaka ieleweke.

Taarifa hii imetolewa na;

Balozi Herbert E. Mrango
KATIBU MKUU (AFISA MASUHULI)
WIZARA YA UJENZI

3. MH.FREEMAN MBOWE - MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI
https://www.youtube.com/watch?v=j0xaIuEaX18

4. MH.JOHN CHEYO - MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI
https://www.youtube.com/watch?v=QlYkNuLVNK8

5. MH.FELIX MKOSAMALI - AUNGA MKONO HOJA WIZARA YA DR.MAGUFULI
https://www.youtube.com/watch?v=QNtrNZKEIy4

Haya kazi twende!!!!
Posted by : Mahebe
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs