Kukiwa kunaelekea ukingoni kufikia tarehe ya mwisho kwa taasisi kupeleka maoni yao katika tume ya Katiba yanayohusu rasimu ya katiba mpya, wadau wengi wangependa kuwepo kwa mdahalo maalum wa wazi baina ya vyama vikuu viwili hapa Tanzania, CCM na CHADEMA utakaorushwa moja kwa moja kupitia Radio au Luninga.
Lengo likiwa ni kuwapa wananchi wengi zaidi fursa ya kuweza kusikiliza, kupima, kuchambua na kuelewa vizuri nini msingi wa misimamo ya vyama hivyo katika maoni yao katika mchakato wa kuandikwa katiba mpya.
Posted by : Tanganyika TANU
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII