PHOTOS : WEMA ALIPOGEUKA KIVUTIO KIKUUBWA MAHAKAMANI

KESI ya kudaiwa kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao Meneja wa Hoteli, Goodluck Kuyumbu inayomkabili Staa wa Filamu, Wema Isaac Sepetu imeunguruma Jumatano iliyopita katika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar na watu kufurika pomoni, Ijumaa linakumegea kilichojiri.
ATINGA NA MSAFARA
Wakati wa kuwasili mahakanai hapo, Wema aliambatana na msafara wa magari matatu, yeye akiwa katika lake la aina ya Audi Q 7, magari mengine yalikuwa ni Toyota Opa na Toyota Hiace yaliyokuwa na watu wake.
Kutokana na jamii kupenda kufuatilia matukio ya kila siku ya Wema, watu kibao walifika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo.
Mara baada ya mlimbwende huyo wa mwaka 2006-07 kuzama katika chumba cha mahakama, kulitokea vurugu kwa baadhi ya watu kukanyagana ili kutaka kumuona na kusikilza kesi hiyo kwa ukaribu zaidi.
Wema aliingizwa katika chumba cha mahakama sambamba na Goodluck ambapo Hakimu Bernice alianza kumuuliza mlalamikaji kama alikuwa na mashahidi walioshuhudia tukio hilo lilivyotokea.
Goodluck alijibu kuwa anao mashahidi na kumwambia hakimu kwamba anaweza kuwaleta mbele ya mahakama hiyo.
Hakimu aliamuru kesi hiyo iahirishwe hadi Agosti 20, mwaka huu na kumtaka mlalamikaji kufika na mashahidi wake.
Kuonesha kwamba watu wengi walikuwa wamefika kushuhudia kesi hiyo, walitawanyika baada ya uamuzi huo.
WEMA ANUNUA MIHOGO
Mara baada ya kutoka mahakamani na kuruhusiwa kuondoka kutokana na dhamana aliyonayo, Wema alionekana akinunua mihogo kwa ajili ya futari ya siku hiyo.
Views: 1725
I usually do not leave a bunch of comments, but I read a ton of remarks here "PHOTOS : WEMA ALIPOGEUKA KIVUTIO KIKUUBWA MAHAKAMANI".
ReplyDeleteI actually do have some questions for you if it's
okay. Could it be simply me or does it give the impression like some of these remarks come across like they are coming from brain
dead people? :-P And, if you are writing at other sites,
I would like to keep up with anything fresh you have to
post. Would you post a list of every one of all your public sites like your twitter feed, Facebook page or linkedin profile?|
Here is my web page ... pity 2014 program (http://nowyprogrampity2014.pl)