PICHA : KILICHOJIRI KATIKA MAZISHI YA BILIONEA ERASTO MSUYA JANA....
zikiwa
ni siku takribani sita zimepita tangu mfanyabiashara wa madini ya
Tanzanite aliyefahamika kwa jina la Erasto Msuya kupigwa risasi zaidi ya
ishirini na kufariki dunia papo hapo katika eneo la Bomang'ombe karibu
na njia panda ya KIA).
Kifo hicho kilichokua na utata mkubwa na kupelekea watu wengi kujiuliza
maswali mengi yasiokua na majibu. Leo ilikua ni siku ya mazishi ya
mfanyabiashara huyo ambaye kutokana na kuwa alikua akiishi jijini Arusha
maeneo ya kwa Iddi ilibidi jana jumatatu wafanye utaratibu wa kuuga
mwili wa marehemu nyumbani kwake na leo jumanne kwenda kuzikwa Mirerani
katika kijiji cha Kairo.
Msiba wa Erasto ulikua ni gumzo
kubwa sana na watu wamekiri hawajawai kuona msiba kama huu maana
kilichokua kikiwashangaza watu ni jeneza lililokua likifunguliwa kwa
rimoti, na pia ni mazishi yaliyokua na watu wengi sana. Kila kona
kulikua na minong'ono ambayo ilikuwa ikizungumzia utata wa kifo chake.
Kamati ya maandalizi ya mazishi wakishirikiana na ndugu, jamaa na
marafiki walijitahidi sana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa maana
haikuwa kazi rahisi kuweza kumudu kuhakikisha usalama wa wingi wa watu
uliokuwepo katika mazishi ya Erasto.
Wakati unaingia nyumbani kwa bilionea Erasto Msuya hili ndio bango lililokua limewekwa.
Hapa utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Maremu Erasto Msuya.
Hii ndio nyumba ya milele ya bilionea Erasto Msuya ikiandaliwa.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII