UJUMBE WA BIRTHDAY KUTOKA KWA NISHA KWENDA KWA HEMED WAZUA MASWALI....SOMA ALICHOKIANDIKA
Leo mwigizaji Hemedi Suleiman maarufu kama Hemedy PHD anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 27 katika ulimwengu huu.
Huku akimiminiwa salamu nyingi sana za pongezi na fans na wadau mbalimbali nchini. Moja ya salamu zilizomfikia mkali ni kutoka kwa mwanadada Nisha Jabu, ambaye aliamua kufunguka yafuatayo na kuacha watu wakiwa na maswali bila majibu kuhusu alichokiandika.
“HAPPY BIRTHDAY.. mwanaume unaefanana na mwanaume wa maisha yangu, mwanaume nnaempenda kuliko chochote duniani,mwanaume alienifanya nisione mwingine duniani zaidi yake,mwanaume akiyenipunguza kilo kumi ndani ya siku 20,(mind ur own bizzness usiniulize kwanini), ninapokuangalia ww namuona yeye,, HAPPY BIRTHDAY my Lusungu my Fernandoo .. my Mathias,, maisha mema na yenye baraka tele yawe mbele na nyuma yako..”
Huo ni ujumbe alioundika mwanadada huyu kwa Hemedy.
Happy birthday Hemedy.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII