HUKU
kukiwa na madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui amekamatwa na
kufungwa nchini Brazil kwa kunaswa na unga, mwanadada huyo ameibuka na
kufafanua juu ya tuhuma hizo. Akizungumza
na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu kutokea
Brazil, Aisha alisema ameshangazwa na madai hayo wakati yeye yuko nchini
humo akiwa amemfuata mchumba wake ambaye jina lake hakuwa tayari
kulianika.
“Jamani
hayo madai ya kwamba nimefungwa huku kwa kesi ya madawa ya kulevya mimi
mwenyewe nayashangaa. Niko huku kwa mwezi wa nne sasa, nimekuja kwa
mchumba wangu. Hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi
unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu.
“Wakati
naondoka Tanzania ilikuwa kimyakimya kwa kuwa nilijua kuna baadhi ya
watu watazusha mambo ya kunipaka matope na ndicho walichokifanya. “Naomba
Watanzania wajue niko huru kabisa, naendelea na shughuli zangu kama
kawaida. Natarajia kurudi Bongo hivi karibuni,” alisema Aisha.
Kwa hisani ya GPL
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII