Siku chache baada ya kunyakua dola za kimarekani laki tatu, USD 300,000 katika shindano la BBA, Mshindi wa shindano hilo Dilish Mathew ameingia katika wakati mgumu baada ya mwanaume mmoja kutoka kenya kudai kuwa yeye ndio baba mzazi wa Mrembo huyo. Abdi Guyo anadai kuwa Dilish ni mwanaye na aliyaongea hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha Television kimoja nchini Kenya. Inawezekana ikawa ni kweli au la lakini mama yake Dilish ndio mwenye uthibitisho, Dilish mwenyewe aliwahi kukaririwa akisema kuwa baba yake ni Msomali na hajawahi kumwona. SO WHO KNOWS INAWEZEKANA PIA IKAWA NDIO HUYU
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII