IRENE UWOYA NA SHIGONGO WAENDELEA KUVUTANA MASHATI.....SOMA ALICHOKISEMA UWOYA KUHUSU SHIGONGO

Irene Uwoya na Shigongo “kazi ipo”; Irene aapa  “kumfanyia mbaya” shigongo, asema ipo siku atasema ukweli wote
Lile bifu linalondelea kati ya mwigizaji Irene Uwoya na mmiliki wa kampuni maarufu ya magazeti nchini Erick Shigongo limeshika hatamu mpya baada ya mwigizaji huyo kuendelea kusema yake ya moyoni kuhusu kile ambacho anakisema kuendelea kuchafuliwa na mfanyibiashara huyo kupitia magazeti yake hayo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii Irene ameandika...
“…Ipo siku ntaongea ukweli kuhusu shigongo na ushaid pia ntatoa...usilo lijua nikama usiku wagiza ndomana atawadanganya wasio na akili na wasio mjua....ntapgana nae mpaka tone la mwisho la damu yangu ntasema kila kitu kwanin ananichukia...na ntaweka kila kitu waz....den wenye akili watajua naongea nin...simuogop atakama atanichafua kiasi gan...hizo kwangu ni matone yamvua bado mvua yenyewe...I don care kwaatakae muamin but mwisho wa siku ukweli utaonekana na atataman ardhi ipasuke......mim irene uwoya sijashawishiwa na mtu wala kulazimishwa nahaaidi ya kwamba ntaongea…”
Hayo ni maneno ya mwanadada huyu kuhusu linachoendelea kati ya na Erick Shigongo.
Baadaye tutafanya mawasiliano na Irene Uwoya ili tuweze kuwaletea undani halisi wa sakata hili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs