Van Vicker muigizaji kutoka Ghana ambaye anafanya vizuri hadi nchini Nigeria ameingia Tanzania jumapili iliyopita na anaondoka leo tarehe 19/9 kurudi kwao Ghana. Hashimu Kambi ambaye ndiyo mwenyeji wake akiongea na millardayo.com alisema,”Van Vicker amekuja Tanzania kuigiza movie yangu ambayo mwanzoni niliipa jina la The Network. Lakini kutokana na kuwa kuna movie nyingine ambayo imetoka na jina hilo hilo nimeamua ku-change jina. Hadi sasa nina majina manne bado sijaamua kutumia lipi.”
Hashimu Kambi aliendelea,”Vicker amefika hapa Tanzania jumapili na anamalizia baadhi ya scene leo na ataondoka leo usiku tare 19/9. Kazi ikiwa tayari tutawaambia inavyotoka na watanzania wasubili kitu kizuri kwasababu kwenye hii movie kuna watu kama Vicker mwenyewe,Weru Sengo,Irene Paul na wengine. So, itakuwa kazi nzuri sana”
Van vicker anaonekana kufurahia kuwa Tanzania kwasababu amekuwa akipiga picha sehemu nyingi sana anazokuwa.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII