YALIYOJIRI KATIKA IBADA YA KUMUAGA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA
Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wamejitokeza kwa wingi katika kumuanga SHUJAA WA INJILI Dr Moses Kulola aliyefariki 29 Agosti saa 5.30 hapa jiji Dar.
Kati ya watu ambao wamekuwepo katika ibada hii ya kuuaga mwili wa Dr Askofu Moses Kuloa, wamehuduria watumishi wa Mungu mbalimbali ikiwa ni pamoja na maaskofu wainjilisti mitume na manabii.
Askofu kulola alizaliwa mkoani Mwanza, mwaka 1930 na kufariki 29 agost 2013.
Baadhi ya watumishi
Katika uhai wake mzee Kulola alifanya kazi ya Injili hadi kifo
kinamchukuwa, ila kati ya kazi aliyoifanya ni pamoja na kutembea kwa
mguu kutoka Mza hadi Mtwara. Lakini pia safari nyingi alizozifanya
zilikuwa katika mazingira magumu. Amehubiri injili ndani na nje ya nchi.
Mama Kulola (Mjane
Mtoto wa Mzee Kulola Willy, akilia kwa uchungu
Askofu Silvester Gamanywa akimpa pole mama Kulola
Watumishi wa Mungu mbalimbali wakisubiria mwili wa Dr Moses Kulola
Msafara wa mwili wa marehemu Dr Mose Kulola ukiwasili katika viwanja vya Temeke
Waimbaji mbalimbali walikuwepo
Baadhi ya ndugu kutoka Mza
Mchungaji Lwakatale akiandika kwenye kitabu cha waombolezaji
Watumishi wengi walifika kwa ajili ya kuuaga mwilia wa aliyekuwa shujaa wa Injili Tz Dr Moses Kulola
Mchungaji Getrude Lwakatare wa Mikocheni Asb. of God
Mchungaji Antony Lusekelo
Askofu Silvester Gamanywa
Watumishi wengi mbalimbali waliopata nafasi
ya kuelezea jinsi walivyomfahamu Dr Kulola, walisifu jinsi alivyokuwa
akipiga injili isyokuwa na ubaguzi wala upendeleo.
Miongoni mwa watu waliofika na kueleza jinsio walivyomfahamu Mzee Kulola ni ni Katibu mstaafu wa CCM
Filip Mangula, ambaye amekuwa msaada mkuubwa katika maisha yake ya kazi. Na hata akampa mtoto wake jina la mzee kulola ( Moses)
Lakini pia kwa niaba ya jeshi la polisi,
Adivela Senso ameeleza jinsi Mzee Kulola alivyoweza kulisaidia jeshi la
Polisi pindi yanapotokea matukio ya ki ualifu, na mzee alienda sehemu
zenye shida na kufanya mikutano ya injili.
Anthony Joseph mtangazaji wa WAPO Radio akitoa heshima zake za mwisho, nyuma ni Obedy Kikao mtangazaji wa Upendo FM radio
Ilikuwa ni siku ya Watumishi wa Mungu kukutana pamoja
Viongozi wa chama na selikari nao pia walikuja kuaga shujaa wa Imani
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Adivera Senzo aliliwakirisha jeshi hilo katika msiba huu mkubwa
Makamu wa Rais Gharib Bilali akiwasiri katika kanisa la EAGT tayari kwa ajili ya kuja kutoa heshima za mwisho.
Askofu Silvester Gamanywa akiteta jambo na katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dr. Wilbrod Slaa
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII