Pages

Sunday, October 27, 2013

BAADA YA KUTOKEA HITILAFU YA UMEME JANA FIESTA DAR.....WASANII WAKUBWA WATAPAFORM LEO JIONI, BUREEEEEEEE




Kutokana na kutokea hitilafu ya umeme Alfajiri ya leo kwenye show ya Serengeti Fiesta Dar, iliyopelekea baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajia kupanda jukwaani kutumbuiza akiwemo Davido, Mohombi, Diamond, Nay wa Mitego na wengine kushindwa kupanda, leo kuanzia saa tisa, wasanii hao watapanda tena jukwaani kuzikonga nyoyo za mashabiki wao bila kiingilio chochote.
 
Ni katika uwanja ule ule, jukwaa lile lile la Serengeti Fiesta Dar es Salaam ambapo Diamond,Davido,Mohombi pamoja na Nay wa Mitego watapanda kuanzia saa 9 jioni mpaka saa 12.Show hiyo ya bure itapambwa pia na bendi ya Twanga Pepeta.
-Habari kwa hisani ya bongo5

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII