Mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha ITV na Radio
One, Ufoo Saro amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na mtu aliyefahamika
kwa jina la Anthery Mushi.
Mushi ambae ameelezwa kuwa alikuwa mchumba wa Ufoo aliyekuwa anafanya kazi katika shirika la Umoja wa mataifa, pia alimpiga risasi mama mzazi wa Ufoo na kumuua kisha akajiua kwa kujipiga risasi.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya kinondoni, Camilius Wambura amesema tukio hilo lilitokea leo majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi maeneo ya Kibamba CCM, Wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Kamanda Wambura amesema polisi bado wanaendelea na uchunguzi, lakini taarifa za awali zinaonesha kuwa Mushi alirejea kutoka Sudan ambapo ndipo kilipo kituo chake cha kazi, na alielekea maeneo ya Kibamba kwa mama yake Ufoo Saro, na alipofika huko alimpiga risasi kifuani mama Saro na kumuua na kisha kumpiga Ufoo na kujipiga risasi juu ya kidevu na kufariki dunia. Ufoo alikimbizwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Nae mkuu wa upeleezi kanda maalum ya Dar es salaam, Hemed Msangi amesema Ufoo alipigwa risasi tumboni na begani. Alisema anaendelea vizuri na kwamba madaktari wanahangaika kuhakikisha wanaokoa maisha yake.
Taarifa ambazo bado hazijathibishwa zinasema kuwa baada ya Mushi kupeleka malalamishi yake kwa mama Saro, mama aliegemea upande wa mwanae wakati wakiwa wote watatu hali iliyomsababisha Mushi kuchukua maamuzi hayo yasiyo ya kawaida.

No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII